In Summary

• Negreira amewaambia wachunguzi kwamba hakuwapendelea Barcelona katika maamuzi yoyote ya waamuzi.

• Forbes wanadai kwamba wanaweza kukabiliwa na kushushwa daraja kutoka kwa La Liga au kuwa na pointi zao.

Barcelona wajipata pabaya kwa kumhonga refa
Image: Facebook

Kilabu ya Barcelona kutoka Uhispania imekuwa ya tatu katika timu kubwa za Ulaya kukumbwa na skendo za kutishia kushushwa daraja au kupokonywa pointi kadhaa.

Baada ya Juventus kujipata katika joto hilo na kupokonywa pointi 15, kesi dhidi ya Manchester City ingali inaendelea huku adhabu ikitajwa kuwa huenda watashushwa daraja kutoka ligi ya premia au kupokonywa pointi.

Barcelona nao wameingia kwenye sakata hilo baada ya kudaiwa kulipa mamilioni ya pesa kwa makamu wa rais wa marefa nchini Uhispania ili kupata matokeo ya upendeleo.

Kulingana na jarida la GiveMe Sport, Barcelona walimlipa naibu rais Jose Maria Enriquez Negreira kima cha pauni milioni 1.4 kati yam waka 2016 hadi 2018.

Negreira alikuwa makamu wa rais wa Shirikisho la Soka la Uhispania kutoka 1994 hadi 2018. Barca wametuhumiwa kufanya malipo matatu kwa DASNIL 95 SL: €532,728.02 mwaka 2016, €541,752 mwaka 2017 na €318,200 mwaka 2018.

Malipo yalisimamishwa mnamo 2018, mwaka ambao Negreira aliacha jukumu lake kama makamu wa rais wa Kamati ya Waamuzi ya RFEF.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka inachunguza madai hayo.

Negreira amewaambia wachunguzi kwamba hakuwapendelea Barcelona katika maamuzi yoyote ya waamuzi.

Badala yake amedai alitoa ushauri wa mdomo kwa klabu katika masuala mengi ikiwa ni pamoja na jinsi wachezaji wanavyopaswa kujiendesha mbele ya waamuzi.

Barcelona wanaweza kukabiliwa na adhabu kali iwapo watapatikana na hatia ya kufanya makosa. Forbes wanadai kwamba wanaweza kukabiliwa na kushushwa daraja kutoka kwa La Liga au kuwa na pointi zao.

 

View Comments