In Summary

• Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Gabriel Martinelli, 21, pia alikubali mkataba mpya wa muda mrefu mwezi Februari.

Bukayo Saka made his Arsenal first-team in debut in November 2018
Image: BBC

Nyota wa Uingereza Bukayo Saka anakaribia kusaini mkataba mpya na vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Arsenal.

Kulingana na duru nchini Uingereza mazungumzo yanaendelea kuhusu mkataba mpya, ambao bado haujatiwa saini, lakini hisia ni kwamba makubaliano yamekaribia.

Saka, 21, ni mmoja wa wachezaji nguzo uwanjani Emirates, akiwa amefunga mabao tisa na kusajili pasi nane za mabao katika mechi 23 za ligi huku Arsenal wakiwania ubingwa.

Mkataba wa Saka ulipaswa kuisha mwaka 2024.

Saka ambaye asili yake ni Afrika Magharibi alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha kwanza cha Arsenal mnamo Novemba 2018, baada ya kujiunga na chuo cha mafunzo ya soka cha Hale End akiwa na umri wa miaka saba.

Mkataba huo mpya, unaoripotiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 10 kwa mwaka na unaomweka katika klabu hiyo hadi 2028, utaipa Arsenal nguvu zaidi wakiwinda taji la kwanza la ligi baada ya miaka 19.

Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Gabriel Martinelli, 21, pia alikubali mkataba mpya wa muda mrefu mwezi Februari.

Vijana wa Mikel Arteta, ambao wako pointi mbili mbele ya mabingwa watetezi Manchester City, watakuwa ugenini Leicester Jumamosi.

View Comments