logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Folarin Balogun: Mshambuliaji wa Arsenal afanya mazungumzo ya kuichezea Marekani

Hapo awali alisema atakuwa tayari kuiwakilisha Nigeria.

image
na Radio Jambo

Makala24 March 2023 - 12:52

Muhtasari


•Kocha Hudson anasema mazungumzo yamefanyika na Folarin Balogun kuhusu mshambuliaji huyo kubadili utaifa na kuchezea Marekani.

•Balogun ameichezea Uingereza katika timu nne tofauti za vijana. 

Kocha wa muda wa Marekani Anthony Hudson anasema mazungumzo yamefanyika na Folarin Balogun kuhusu mshambuliaji huyo kubadili utaifa na kuchezea taifa hilo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alizaliwa Marekani kwa wazazi kutoka Nigeria lakini alikulia Uingereza, na anaweza kuchezea nchi yoyote kati ya hizo tatu.

Balogun, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Ufaransa ya Reims akitokea Arsenal, ameichezea Uingereza katika timu nne tofauti za vijana. Alijiondoa kwenye kikosi cha England cha Under-21 wiki hii kutokana na majeraha.

"Kama nilivyosema hapo awali, tumekuwa na mazungumzo," alisema Hudson. Balogun ameifungia Reims mara 17 kwenye Ligue 1 msimu huu na yuko nyuma kwa mabao mawili tu nyuma ya wafungaji wanaoongoza kwa ufungaji katika liigi hiyo Kylian Mbappe na Jonathan David.

Hapo awali alisema atakuwa tayari kuiwakilisha Nigeria na bado ana chaguo la kuchezea nchi gani kwani hajachezea timu ya wakubwa ya England kiushindani.

Timu ya Marekani imekuwa Florida ikijiandaa kwa mchezo wa Ligi ya Mataifa ya Concacaf huko Grenada siku ya Ijumaa. Hudson alisema: "Tumezungumza [na Balogun]. Yeye yuko hapa akiwa na mapumziko kidogo na kisha mazoezi, na tumekuwa na majadiliano kadhaa.

"Nadhani imekuwa nzuri kwa sababu imekuwa fursa kwetu na yeye kujua kuhusu programu yetu na sisi ni nani na tunafanya nini na ndivyo hivyo. Natumai tutapata nafasi ya kuzungumza naye tena. "Imekuwa nzuri na najua wachache wamezungumza naye pia."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved