In Summary

• Weah aliweka rekodi hiyo miaka kadhaa iliyopita akiwa kama mchezaji wa AC Milan.

• Kwa sasa Weah ni rais wa Liberia baada ya kustaafu kandanda.

George Weah ammiminia sifa Victor Osimhen kwa kuvunja rekodi yake Serie A.
Image: Twitter, Facebook

Rais wa Liberia George Weah ambaye alikuwa mchezaji wa Seria A enzi hizo amempongeza mshambuliaji wa sasa wa Napoli, Mnigeria Victor Osimhen kwa kuvunja rekodi yake ya ufungaji mabao katika igi hiyo kwa wachezaji wa Kiafrika.

Osimhen alifunga bao la ushindi la Napoli dhidi ya Fiorentina siku mbili zilizopita na kuiwezesha timu hiyo kutawazwa mabingwa wa Serie A msimu huu baada ya miaka 33.

Bao hilo, ambalo ni la 23 kwake msimu huu ni bao lake la 47 katika Serie A, akimpita Weah (mabao 46) na kuwa mfungaji bora zaidi wa Kiafrika katika ligi kuu ya Italia.

Weah alimsherehekea Osimhen na kumpoa hongera akimwambia kuwa si jambo rahisi kuvunja rekodi hiyo ambayo imekuwa ikisimama kwa muda mrefu.

“Ninajivunia ushujaa wako na ninakupongeza kwa mafanikio haya ya ajabu ambayo ni matokeo ya bidii yako, bidii na uvumilivu. Nimefurahishwa pia na maneno yako mazuri ya heshima kwa heshima kwangu baada ya kufikia hatua kubwa kama hii,” Weah alisema.

Hata hivyo, Weah alimuusia kutolaza damu kwani bado ni kijana mdogo na akiendelea kujituma ataweka rekodi nyingine Zaidi ambazo zitawapa vijana wa siku za usoni kibarua kigumu kizifikia na kuzipiku.

“Hata hivyo, nataka kuwaonya msiridhike. Kuna rekodi zangu nyingi zaidi kwako kuvunja. Nakutakia uendelee kufikia mafanikio makubwa zaidi. Nasubiri Bao lako la 100 katika mashindano yote nchini Italia ili uweze kusherehekea (lakini usivue shati lako kama nilivyofanya au utapata Kadi ya Njano),” Weah alishauri.

“Rekodi nilizoweka hazikusudiwa kama changamoto, lakini kama motisha kwako na kwa Wachezaji wengine wa Kiafrika. Tuna vipaji bora zaidi. Unapaswa kubaki mnyenyekevu, mstahimilivu na mwenye umakini. Usikengeushwe,” Weah aliongeza.

View Comments