In Summary

• Ushindi huo uliwasongesha alama 11 kutoka nafasi ya tatu zikiwa zimesalia mechi tatu. Hii ina maana, timu iliyo nafasi ya tatu haiwezi kumpita Shabana au Seal.

• Hii itakuwa mara ya kwanza kwa timu ya Murang’a Seal kushiriki ligi kuu ya taifa.

Wachezaji wa timu ya Shabana FC.
Image: TWIITER/SHABANA FC

Shabana FC na Murang’a Seal Jumapili zilipanda daraja hadi Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka la Kenya (KPL) kwa msimu mpya wa 2023-2024.

Hii ni baada ya pande zote mbili kushinda mechi zao za National Super League (NSL) ambazo ziliwafanya wasonge mbele hadi pointi 64 kila mmoja.

Ushindi huo uliwasongesha alama 11 kutoka nafasi ya tatu zikiwa zimesalia mechi tatu. Hii ina maana, timu iliyo nafasi ya tatu haiwezi kumpita Shabana au Seal.

Shabana waliwaondolea matumaini ya kupandishwa daraja timu ya Migori Youth baada ya kuwachapa bao moja komboa ufe.

Mechi  hiyo ilishudhudia ghasia uwanjani Gussi baada ya mashabiki wa Migor Youth kuhisi ni kama mwamuzi alikuwa akiipendelea timu ya Shabana.

Mechi hiyo ilihudhuriwa na viongozi kadhaa wa Kaunti ya Kisii akiwemo Mbunge wa Mugirango Kusini Sylvanus Osoro na aliyekuwa waziri wa Michezo wa Kaunti ya Kisii Duke Mainga.

Seal pia ilisajili ushindi sawa na wenzao Shabana walipowalemea klabu ya Coastal Heroes FC katika uga wa Mbaraki Stadium mjini Mombasa.

Ali Yusuf alifunga bao hilo muhimu katika dakika za kuongeza katika kipindi cha kwanza, faida ambayo walilinda kipindi cha pili na kuibuka na alama zote tatu.

Mjini Kisii, bao la dakika ya tatu kutoka kwa winga wa Shabana Isaac' Otieno ndilo pekee timu inayonolewa na Sammy Okoth ilihitaji kuwashinda Migori Youth na kuwapandisha daraja hadi FKF-PL.

Shabana wanarejea katika ligi kuu ya KPL kwa mara ya kwanza tangu kushushwa daraja mwaka wa 2006.

Hii itakuwa mara ya kwanza kuwa timu ya Murang’a Seals kushiriki ligi kuu ya taifa.

Wanahabari na washikadau wa soka nchini walichukulia timu hizi mbili kupanda daraja kuwa ushindi mkubwa katika sekta ya kabumbu nchini kwani timu hizi mbili zinawakilisha maeneo nje ya kaunti ya Niarobi.

View Comments