logo

NOW ON AIR

Listen in Live

ManCity yajiondoa katika mbio za kumsaini Rice baada ya Arsenal kuwapiga mkwara

Nahodha wa The Hammers aliongoza chati za ligi kuu ya Uingereza linapokuja suala la kukatiza.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri28 June 2023 - 10:21

Muhtasari


• West Ham na Arsenal wanapanga kuingia katika mazungumzo zaidi leo huku wakitarajia kufikia makubaliano juu ya muundo wa uhamisho huo.

• Manchester City haitalingana na ofa ya Arsenal ya pauni milioni 105 kumnunua Declan Rice, kwa mujibu wa Manchester Evening News.

ManCity yajiondoa katika mbio za kumsaini Declan Rice.

Manchester City wamejiondoa kwenye mbio za kutaka kumsajili nahodha wa West Ham Untied Declan Rice kufuatia Arsenal kutoa ofa ya pauni milioni 105 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza.

Manchester City haitalingana na ofa ya Arsenal ya pauni milioni 105 kumnunua Declan Rice, kwa mujibu wa Manchester Evening News.

The Gunners waliona ofa mbili kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza zikakataliwa na West Ham, ya kwanza ikiwa na thamani ya pauni milioni 75, pamoja na nyongeza ya pauni milioni 15.

City kisha waliingia rasmi kwenye kinyang'anyiro hicho Jumatatu usiku kwa dau lao, ambalo pia lilikataliwa na Wagonga nyundo.

Siku ya Jumanne jioni, klabu hiyo ya kaskazini mwa London iliongeza dau, na kuwasilisha ombi la rekodi ya klabu yenye thamani ya pauni milioni 100 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 5, football.london iliripoti.

Ofa hiyo inasemekana ilisababisha City kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, jambo ambalo ni msukumo mkubwa kwa Mikel Arteta na Arsenal wanapojaribu kupata mlengwa wao nambari moja.

Katika miaka ya hivi karibuni, Rice amejidhihirisha kuwa mmoja wa wachezaji wanaoshikilia nafasi ya kati kwenye Ligi Kuu. Nahodha wa The Hammers aliongoza chati za ligi kuu ya Uingereza linapokuja suala la kukatiza, na kusajili 63, kulingana na fbref.

West Ham na Arsenal wanapanga kuingia katika mazungumzo zaidi leo huku wakitarajia kufikia makubaliano juu ya muundo wa uhamisho huo na urefu wa malipo ya ada iliyopangwa ya £100m suala lililosalia, football.london inaelewa.

Wakati meneja wa Arsenal Mikel Arteta alipoulizwa kuhusu kikosi chake kumnasa Rice, alikataa kushawishika kuzungumza kuhusu kiungo huyo mwenye ugumu wa kukaba.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved