logo

NOW ON AIR

Listen in Live

David de Gea athibitisha kuondoka Manchester United baada ya miaka 12

De Gea anaondoka Manchester United msimu huu wa joto, akisema "ni wakati mwafaka wa kukabiliana na changamoto mpya".

image
na Radio Jambo

Makala09 July 2023 - 04:57

Muhtasari


•De Gea alikuwa mchezaji huru kwani kandarasi yake katika klabu hiyo ya Old Trafford ilikuwa imefikia kikomo mwezi uliopita.

•"Sasa, ni wakati mwafaka wa kuchukua changamoto mpya, kujisukuma tena katika mazingira mapya," alisema.

David de Gea kuondoka Man U

Mlindalango wa Uhispania David de Gea anasema anaondoka Manchester United msimu huu wa joto, akisema "ni wakati mwafaka wa kukabiliana na changamoto mpya".

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuwa mchezaji huru kwani kandarasi yake katika klabu hiyo ya Old Trafford ilikuwa imefikia kikomo mwezi uliopita.

De Gea amekuwa United kwa miaka 12 na alicheza katika mechi 545.

"Nilitaka tu kutuma ujumbe huu wa kuwaaga mashabiki wote wa Manchester United," aliandika katika chapisho la mtandao wa kijamii.

De Gea alianza soka lake akiwa Atletico Madrid, lakini alijiunga na United kwa £18.9ml mwaka 2011.

Aliongeza: "Ningependa kutoa shukrani zangu zisizo na shaka na shukrani kwa upendo wa miaka 12 iliyopita. Tumefanikiwa mengi tangu mpendwa wangu Sir Alex Ferguson aliponileta katika klabu hii.

"Niliona fahari ya ajabu kila nilipovaa fulana hii, kuiongoza timu, kuiwakilisha taasisi hii, klabu kubwa zaidi duniani ilikuwa ni heshima inayotolewa kwa wanasoka wachache waliobahatika.

"Kimekuwa kipindi kisichosahaulika na chenye mafanikio tangu nilipokuja hapa. Sikufikiria kutoka Madrid nikiwa kijana mdogo tungefikia kile tulichofanya pamoja.

"Sasa, ni wakati mwafaka wa kuchukua changamoto mpya, kujisukuma tena katika mazingira mapya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved