logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Barcelona wabaki mayatima uwanja wao wa kihistoria Camp Nou ukibomolewa - video

Uwanja huo mashuhuri unapata mabadiliko kidogo katika msimu wa joto.

image
na Davis Ojiambo

Michezo11 July 2023 - 06:03

Muhtasari


  • • Klabu hiyo ilianza mchakato mrefu wa kuboresha uwanja wao mwishoni mwa msimu uliopita.
  • • Barca itacheza mechi za nyumbani za msimu ujao kwenye Uwanja wa Olympic mjini Montjuic.
Uwanja wa Barcelona wabomolewa

Timu ya Barcelona italazimika kutafuta uwanja mbadala msimu kesho baada ya uwanja wao wa nyumbani Nou Camp ukianza kubomolewa tayari kwa ukarabati.

Katika video moja ambayo imepakiwa na jarida la Mundo Deportivo kwenye ukurasa wao wa Twitter, inaoehsa mashine nzito zikibomoa uwanja huo wenye historia ndefu ya klabu hiyo miamba wa Uhispania.

Uwanja huo mashuhuri unapata mabadiliko kidogo katika msimu wa joto na mchakato huo ulianza siku ya Jumatatu wakati mashine zilipoanza kubomoa.

Klabu hiyo ilianza mchakato mrefu wa kuboresha uwanja wao mwishoni mwa msimu uliopita. Barca itacheza mechi za nyumbani za msimu ujao kwenye Uwanja wa Olympic mjini Montjuic.

Hawatarejea kwenye uwanja wao hadi mwishoni mwa 2024, kwani Camp Nou itafunguliwa tena kwa asilimia 70 yenye uwezo wa kuezekea paa na paneli za jua.

Kikosi cha wakubwa kilirejea katika kituo cha mazoezi cha klabu hiyo kwa ajili ya mitihani ya afya siku ya Jumatatu huku wakianza maandalizi yao ya msimu ujao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved