In Summary

• Hermoso awali alitoa taarifa akisema kuwa hakuwa amekubali kupigwa busu na alijihisi kudhalilika kwa unyonge baada ya kitendo hicho.

• Ushiriki wa vilabu vya Uhispania katika mashindano ya Uropa msimu huu unaweza kuwa hatarini kwa sababu ya sakata busu hilo lenye utata.

Rais wa FA Uhispania akosolewa kwa kumpiga busu mchezaji
Image: BBC

Ikiwa ni Zaidi ya wiki moja tangu rais wa shirikisho la soka Uhispania Luis Rubiales kuonekana kwenye kamera akimbusu mwanasoka wa kike Jenni Hermoso kufuatia ushindi wao dhidi ya Uingereza katika fainali za kombe la dunia kwa kina dada, busu hilo la utata limeubua dhana tofauti.

Dhana nyingi ambazo zimeibuka kuhusu busu hilo zimeenezwa na kuvutia maoni tofauti kote ulimwenguni baadhi wakidai kwamba busu hilo lilikuwa ni jambo la kuelewana baina ya Rubiales na Hermoso huku wengine wakisema kuwa busu hilo linapata tope shirikisho la Uhispania na kumtaka Rubilaes kujiuzulu.

Lakini sasa imebainika kwamba busu hilo huenda likaeneza madhara yake hata Zaidi kwa vilabu vya soka vya Uhispania ambavyo vinatarajiwa kushiriki katika mashindano ya Uropa lakini pia madhara hayo yataiathiri hadi timu ya taifa ya Uhispania kuelekea mashindano ya Euro mwakani.

Licha ya kutakiwa kujiuzulu baada ya wachezaji wote wa timu ya taifa kusema hawatoshiriki mecho yoyote mpaka pale atakapojiuzulu, Rubiales mwishoni mwa wiki jana alisisitiza kwamba hatojiuzulu na kusema kuwa busu lilikuwa ni makubaliano ya pande zote – yeye na Hermoso.

Hermoso awali alitoa taarifa akisema kuwa hakuwa amekubali kupigwa busu na alijihisi kudhalilika kwa unyonge baada ya kitendo hicho.

Ushiriki wa vilabu vya Uhispania katika mashindano ya Uropa msimu huu unaweza kuwa hatarini kwa sababu ya sakata busu hilo lenye utata.

Katibu Mkuu wa RFEF ameripotiwa kuitaka UEFA kusimamisha timu za Uhispania kwenye mashindano ya Uropa kwa nia ya kuwalinda Rubiales dhidi ya madai ya serikali kuingilia masuala ya shirikisho hilo.

Iwapo hilo litafanyika, vilabu vya Uhispania katika mashindano ya UEFA vitafukuzwa. Ushiriki wa timu ya taifa ya wanaume katika mechi za kufuzu Euro 2024 pia utabatilishwa.

Real Madrid, Barcelona, ​​Sevilla, Real Sociedad na Atletico Madrid watakosa Champions League, Villarreal na Real Betis hawatashiriki Europa League huku Osasuna wakifukuzwa kwenye Ligi ya Europa Conference.

View Comments