In Summary

•Dirisha la uhamisho wa wachezaji litaendelea kufungwa hadi Januari 2024 ambapo vilabu vitaruhusiwa kununua au kukopa wachezaji.

•Soko lilikuwa na shughuli nyingi zaidi siku ya mwisho ambapo vilabu vilinunua wachezaji wapya, vingine vikachua kwa mkopo au kuuza.

Rob HOlding, Mason Greenwood, Sergio Regulion
Image: HISANI

Dirisha la Uhamisho la Ligi Kuu ya Uingereza hatimaye lilifungwa usiku wa kuamkia Jumamosi, Septemba 2 mwendo wa saa saba usiku.

Hii iliashiria mwisho wa ununuzi na ukopaji wa wachezaji kwa vilabu vya Uingereza baada ya miezi mitatu ya shughuli nyingi sokoni. Dirisha la uhamisho wa wachezaji litaendelea kufungwa hadi Januari 2024 ambapo vilabu vitaruhusiwa kununua au kukopa wachezaji.

Kumekuwa na miondoko mingi ya wachezaji ndani na nje ya vilabu katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Soko lilikuwa na shughuli nyingi zaidi siku ya mwisho ambapo vilabu kadhaa vilinunua wachezaji wapya, vingine vikachua wachezaji kwa mkopo au kuuza.

Hizi hapa ni baadhi ya dili zilizokamilika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho;-

  1. Rob Holding[Arsenal - Crystal Palace] £4m
  2. Sofyan Amrabat[Fiorentina - Manchester United] Mkopo
  3. Albert Sambi Lokonga[Arsenal - Luton] Mkopo
  4. Jonny Evans[Leicester - Manchester United] Huru
  5. Ryan Gravenberch[Bayern Munich - Liverpool] £34.3m
  6. Callum Hudson-Odoi[Chelsea - Nottingham Forest] Haijafichuliwa
  7. Sergio Reguilon[Tottenham - Manchester United] Mkopo
  8. Alex Iwobi[Everton - Fulham] £22m
  9. Andrew Omobamidele[Norwich - Nottingham Forest] £11m
  10. Divock Origi[AC Milan - Nottingham Forest] Loan
  11. Ibrahim Sangare[PSV Eindhoven - Nottingham Forest] Haijafichuliwa
  12. Luis Sinisterra[Leeds - Bournemouth] Mkopo
  13. Jaidon Anthony[Bournemouth - Leeds] Mkopo
  14. Jean-Ricner Bellegarde[Strasbourg - Wolves] Haijafichuliwa
  15. Neal Maupay[Everton - Brentford] Mkopo
  16. Mike Tresor[Genk - Burnley] Mkopo
  17. Brennan Johnson[Nottingham Forest - Tottenham] £45m+
  18. Odysseas Vlachodimos[Olympiakos - Nottingham Forest] Haijafichuliwa
  19. Nicolas Dominguez[Bologna - Nottingham Forest] Haijafichuliwa
  20. James McAtee[Manchester City - Sheffield United] Mkopo
  21. Ansu Fati[Barcelona - Brighton] Mkopo
  22. Clement Lenglet[Barcelona - Aston Villa] Mkopo
  23. Matheus Nunes[Wolves - Manchester City] £55m
  24. Nuno Tavares[Arsenal - Nottingham Forest] Mkopo
  25. Tommy Doyle[Manchester City - Wolves] Mkopo
  26. Cole Palmer[Manchester City - Chelsea] £40m
  27. Altay Bayindir[Fenerbahce - Manchester United] £4.3m

Kimataifa:

  1. Mason Greenwood[Manchester United - Getafe] Mkopo
  2. Joao Cancelo[Manchester City - Barcelona] Mkopo
  3. Remo Freuler[Nottingham Forest - Bologna] Mkopo
  4. Japhet Tanganga[Tottenham - Augsburg] Mkopo
  5. Marc Jurado [Manchester United - Espanyol] Haijafichuliwa
  6. Loic Mbe Soh[Nottingham Forest - Almere City] Mkopo
View Comments