logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Video: Jinsi CR7 alinusurika kadi nyekundu baada ya kumkanyaga golikipa kichwani

Sports Brief waliripoti kwamba Mwamuzi wa kati Glenn Nyberg kutoka Uswidi alimpa kadi ya njano.

image
na Radio Jambo

Habari09 September 2023 - 08:20

Muhtasari


• Kadi ya njano inamaanisha Ronaldo ataukosa mchezo ujao wa Ureno dhidi ya Luxembourg.

Ronaldo akimkanyaga Dubravka.

 Mchezaji wa kimataifa kutoka Ureno ambaye ndiye nambari moja kwa muda wote katika malimwengu ya Soka Christiano Ronaldo alinusurika kuoneshwa kadi nyekundu kaitka mchezo wa usiku wa kumakia Jumamosi baada ya kumkanyaga mlinda lango wa timu pinzani kichwani.

Katika video ambayo imepakiwa mitandaoni, Ronaldo ambaye anaiwakilisha Ureno walikuwa wanacheza dhidi ya Slovakia katika mchezo wa kufuzu michuano ya Euro 2024.

Katika kipindi cha pili Ronaldo alionekana akiteleza chini huku ameinua mguu juu kuelekea kufuma moja kwa moja katika kichwa cha mlinda lango wa Slovakia Martin Dubravka.

Baada ya mapumziko, nahodha wa Selecao, Ronaldo, aligongana na kipa wa Slovakia, Dubravka na hivyo kumuacha akihitaji matibabu. Mpira ulirushwa kwenye eneo hilo, ambalo lilidakwa na mshambuliaji wa Al-Nassr.

Vijana wa Roberto Martinez walichukua uongozi kupitia Bruno Fernandes katika kipindi cha kwanza - bao ambalo lilionekana kuwa tofauti usiku huo huku Ureno wakiendelea na rekodi yao nzuri katika mechi za kufuzu.

Sports Brief waliripoti kwamba Mwamuzi wa kati Glenn Nyberg kutoka Uswidi alimpa kadi ya njano mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38, ambayo aliipokea kwa ustadi. Kisha akazunguka eneo la tukio huku akiangalia hali ya mpinzani wake alipokuwa akipokea matibabu.

 

Wawili hao walikuwa wachezaji wenzake kwa muda mfupi katika klabu ya Manchester United kabla ya mkataba wa Ronaldo kuvunjwa na Dubravka akarudishwa kwa klabu yake kuu, Newcastle United.

Kadi ya njano inamaanisha Ronaldo ataukosa mchezo ujao wa Ureno dhidi ya Luxembourg.

Mapumziko yake ya kimataifa sasa yamekamilika na huenda akarejea Mashariki ya Kati na kusubiri kurejea kwa Ligi Kuu ya Saudia.

Tazama video hiyo hapa;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved