In Summary

• Sheria za UEFA zinasema kuwa timu zinazomilikiwa na mtu mmoja haziwezi kucheza katika mashindano sawa.

• Iwapo United na Nice zote zitafuzu kwa Ligi ya Mabingwa, timu itakayomaliza juu zaidi itacheza, huku nyingine ikipigwa marufuku.

Sir Jim Ratcliffe
Image: BBC SPORT

Manchester United huenda ikapigwa marufuku kushiriki Ligi ya Mabingwa ikiwa ununuzi wa Sir Jim Ratcliffe utatimizwa.

Bilionea huyo wa Uingereza anakaribia kusaini mkataba wa pauni bilioni 1.3 na Glazers kununua asilimia 25 ya hisa za United kupitia kampuni yake, INEOS.

Lakini Ratcliffe tayari anamiliki timu ya Ufaransa ya Nice, jambo ambalo linaweza kusababisha matatizo kwa matumaini ya United kwenye Ligi ya Mabingwa.

Sheria za UEFA zinasema kuwa timu zinazomilikiwa na mtu mmoja haziwezi kucheza katika mashindano sawa.

Iwapo United na Nice zote zitafuzu kwa Ligi ya Mabingwa, timu itakayomaliza juu zaidi itacheza, huku nyingine ikipigwa marufuku.

Gazeti la The Mirror linaripoti kuwa njia pekee ambayo United na Nice zinaweza kucheza Ulaya msimu ujao ni ikiwa moja itafuzu moja kwa moja kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa iliyopanuliwa na nyingine kuingia moja kwa moja kwenye Ligi ya Conference.

Chanzo kimoja cha UEFA kililiambia gazeti la The Sun kwamba hali iko wazi, kwani ni lazima timu zinazodhibitiwa na chama kimoja zizuiwe kuchuana katika mchuano huo, kama ilivyoelezwa na Kifungu cha 5.02 cha kanuni za UEFA.

Iwapo watamaliza katika nafasi sawa, United watafuzu kwa sababu England iko juu kwenye "orodha ya ufikiaji" ya UEFA.

Lakini kufungiwa kwa klabu hiyo ya Old Trafford kutakuja kama nyongeza kwa wapinzani wa Premier League kama vile Arsenal, Tottenham na Chelsea kwani itamaanisha nafasi ya ziada ya Ligi ya Mabingwa itanyakuliwa ikiwa timu ya Erik ten Hag itamaliza katika nafasi nne za juu.

Mapema mwaka huu United na Nice, ambazo kwa sasa ziko nafasi ya sita kwenye Ligi ya premia na pili kwenye Ligue 1 mtawalia, zilipata mwanga wa matumaini.

Rais wa UEFA Aleksander Ceferin alidokeza wakati wa mazungumzo na nahodha wa zamani wa United Gary Neville kwamba sheria zao za umiliki wa vilabu vingi huenda zikalegezwa hivi karibuni.

View Comments