Ligi kuu ya Uhuspania, La Liga kwa kawaida hujumuisha mabishano kadhaa kuhusu nani alisema nini kwa nani kwa msimu, lakini ya hivi punde kati ya mshambulizi wa Real Madrid Jude Bellingham na mwenzake wa Getafe, Mason Greenwood imezua taharuki mtandaoni.
Ili kutatua kesi hiyo, La Liga wameajiri mtaalamu wa kusoma midomo, kwa kimombo lip-reader.
Wakati wa ushindi wa 2-0 wa Real Madrid dhidi ya Getafe siku ya Alhamisi usiku, kamera ya runinga ilionekana kumnasa Bellingham akimwita mchezaji huyo aliyetolewa kwa mkopo na Manchester United ‘mbakaji’.
Getafe waliripoti hili kwa mjumbe wa mechi hiyo, na La Liga wameamua kulichunguza ili kuona kama kuna ushahidi wa kutosha kuliweka kwenye ripoti ya mechi, kama ilivyo kwa Relevo.
Kuanzia wakati huo na kuendelea, inaweza kuchunguzwa na Kamati ya Mashindano, na inaweza kuleta adhabu kwa nyota huyo wa Real Madrid.
Greenwood mwenyewe alitolewa nje mapema msimu huu kwa kumwambia mwamuzi ‘F** off’, kabla ya kadi yake nyekundu kufutwa baada ya kuthibitishwa baada ya mechi ambayo Greenwood aliapa, lakini si kwa mwamuzi.
Mshambulizi huyo wa Getafe hapo awali alituhumiwa kwa jaribio la ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia, kutumia nguvu na unyanyasaji wa nyumbani, lakini mashtaka hayo yalitupiliwa mbali baada ya shahidi mkuu kujiondoa kwenye kesi hiyo.