logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chelsea waivamia na kuipora kambi ya Brighton tena, uvamizi wa 11 ndani ya miezi 17!

Kando na kocha Potter, Chelsea pia wameipora Brighton wachezaji .

image
na Davis Ojiambo

Michezo21 February 2024 - 04:51

Muhtasari


  • • Baada ya kumfuta Thomas Tuchel, Chelsea walimwendea kocha Graham Potter mwaka 2022 na kumfuta kazi miezi michache baadae kufuatia msururu wa matokeo mabaya.
Chelsea na Brighton

Kwa mara nyingine tena, klabu ya Chelsea imeelekeza uvamizi wake katika kambi ya klabu cha Brighton na kuwapora chuma chao, katika msururu ambao umekuwa ukiendelea tangu uongozi mpya wa Chelsea kuchukua usukani.

Taarifa za hivi punde ni kwamba Chelsea wamemkwapua mkuu wa usajili wa Brighton, Sam Jewell – akiwa ni mtu wa 11 kuondoka Brighton na kujiunga na Chelsea katika kipindi cha miezi 17 iliyopita.

Jewell atakuwa sehemu ya mradi wa vilabu vingi chini ya uongozi wa BlueCo kuleta na kuchagua wachezaji wapya wa Chelsea na vilabu Zaidi.

Itakumbukwa kwamba tangu Chelsea wapate uongozi mpya chini ya Todd Boehly, Behdad Eghbali na José E. Feliciano ambao walishikana kikoa kuinunua The Blues kutoka kwa Mrusi Roman Abrahamovic, klabu hiyo imekuwa ikiipora Brighton watu mbalimbali kutoka kwa wachezaji, kocha na hata wafanyikazi wengine.

Baada ya kumfuta Thomas Tuchel, Chelsea walimwendea kocha Graham Potter mwaka 2022 na kumfuta kazi miezi michache baadae kufuatia msururu wa matokeo mabaya.

Kando na kocha Potter, Chelsea pia wameipora Brighton wachezaji Marc Cucurella ambaye ni beki, mlinda lango Robert Sanchez na kiungo ghali Zaidi Moises Caicedo.

Lakini pia walichukua baadhi ya wafanyikazi wao katika klabu wakiwemo Paul Winstanley, Billy Reid, Björn Hamberg, Bruno Saltor, Ben Roberts, Kyle McCauley na sasa, Sam Jewell.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved