In Summary

•Asuza ambaye alijulikana zaidi kama Asuu aliaga dunia katika hali ya kutatanisha mnamo siku ya Jumapili, Machi 17.

•Ghost alishiriki kumbukumbu nzuri ya marehemu akimtaja kama mshambuliaji bora ambaye alisababisha bashasha kwa wengine.

Mtangazaji Ghost Mulee amemuomboleza mwanasoka Joseph Asuza

Mtangazaji wa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi katika Radio Jambo, Jacob ‘Ghost’ Mulee ameomboleza kifo cha mwanasoka wa zamani wa Kenya Joseph Chama Asuza.

Asuza ambaye alijulikana zaidi kama Asuu aliaga dunia katika hali ya kutatanisha mnamo siku ya Jumapili, Machi 17

Huku akimuomboleza kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, mtangazaji Ghost Mulee alishiriki kumbukumbu nzuri ya marehemu akimtaja kama mshambuliaji bora ambaye alisababisha bashasha kwa wengine.

“Joseph Asuza’Asu,’ nakumbuka vipindi vyetu vya mazoezi katika limuru na Red Berets fc katika Ligi Kuu ya Kenya.

Ulikuwa mshambuliaji mzuri na mwenye furaha kuwa naye. Imba na malaika hadi tukutane tena,” Ghost aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Kocha huyo wa zamani wa Harambee Stars aliambatanisha taarifa yake na video ya marehemu Asuu akiburudika katika Milima ya Kyamwilu huko Machakos.

“RIP bro,” aliongeza.

Asuu alichezea klabu ya Red Berets FC katika Ligi Kuu ya Kenya na pia aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Police FC kabla ya kuhamia Marekani.

Ligi Kuu ya FKF pia imemuomboleza mwanasoka huyo wa zamani kwa ikimtambua kama mhusika muhimu katika ulimwengu wa soka.

"Soka la Kenya limepoteza sifa ya kudumu uwanjani na uwanjani, tunatoa pole kwa familia ya mchezaji wa zamani wa Red Beret na kocha msaidizi wa kwanza wa Police FC Joseph "Journeyman Asu" Chama Asuza," ligi kuu ya FKF ilisema katika taarifa yake. .

Kifo cha ghafla cha Asuu kinakuja siku chache tu baada ya mamake kufariki.

View Comments