In Summary

•Timu zote zihakikishe nahodha wao ndiye mchezaji pekee anayezungumza na mwamuzi.

•Hatua ya shirikisho la soka barani Ulaya ni kujaribu kuzuia makundi ya wachezaji "kuwafurusha" waamuzi katika matukio ambayo ni "mbaya kwa taswira ya soka".

Refa Antony Taylor
Image: Facebook

UEFA imeziambia timu za Euro 2024 kuwa manahodha pekee ndio wataruhusiwa kuwasiliana na waamuzi ili kuzungumza juu ya maamuzi yaliyochukuliwa wakati wa michezo na wachezaji wengine wanaofanya hivyo wanaweza kupokea kadi ya majano.

Hatua ya shirikisho la soka barani Ulaya ni kujaribu kuzuia makundi ya wachezaji "kuwafurusha" waamuzi katika matukio ambayo ni "mbaya kwa taswira ya soka".

"Katika nia ya kuboresha hali ilivyo sisi Uefa tunataka waamuzi kueleza zaidi maamuzi yao kwa timu zote zinazoshiriki michuano ya Uefa Euro 2024," alisema Roberto Rosetti, mkurugenzi mkuu wa waamuzi wa Uefa.

"Tutafanyaje hili? Wazo ni rahisi: tunaomba timu zote zihakikishe nahodha wao ndiye mchezaji pekee anayezungumza na mwamuzi.

"Tunaomba manahodha wahakikishe wenzao hawamvamizi na kumzingira mwamuzi, na kuruhusu mazungumzo ya moja kwa moja yafanyike ili uamuzi huo utolewe kwa wakati na kwa heshima."

 

Mpango huo wa Uefa unafuatia wabunge wa kandanda, Bodi ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Ifab), kutangaza majaribio mapema mwaka huu ambayo yalijumuisha nahodha wa timu pekee kuweza kumwendea mwamuzi katika hali fulani.

Euro 2024 itafanyika Ujerumani, ambao wataanza mashindano kwa mchezo dhidi ya Scotland mnamo Ijumaa, 14 Juni.

"Mchezaji mwenzake yeyote anayepuuza nafasi ya nahodha wake na/au anayemkaribia mwamuzi akionyesha dalili zozote za kutoheshimu au kutokubali ataonyeshwa kadi ya njano," aliongeza Rosetti.

"Ni dhahiri, ikiwa nahodha ni golikipa, kutakuwa na haja ya kuwa na mchezaji wa nje aliyeteuliwa ambaye anaweza kutimiza jukumu hili endapo tukio litatokea upande wa pili wa uwanja."

View Comments