In Summary

•Sambi Lokonga anachukuliwa kuwa ni ziada kwa mahitaji ya Arsenal kutokana na wingi wa vipaji katika safu ya kati

•Vilabu kadhaa vya Ulaya tayari vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Lokonga, ambaye atakaa mapumzikoni wiki chache zijazo.

Sambi Lokonga. Picha;Instagram

Albert Sambi Lokonga anakaribia kuondoka Arsenal msimu huu wa joto baada ya mazungumzo na mkurugenzi wa michezo wa Arsenal,Edu Gaspar.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anachukuliwa kuwa ni ziada kwa mahitaji ya Arsenal kutokana na wingi wa vipaji katika safu ya kati. Klabu pamoja na  mchezaji mwenyewe wamekubaliana kwa faragha kwamba ni bora kwa mchezaji huyo wa zamani wa Anderlecht kutafuta timu nyingine.

Mwaka jana, Lokonga alikuwa kwa mkopo Crystal Palace ambako alitatizika, lakini msimu huu alifurahia mchezo mzuri akiwa Luton ambapo uchezaji wake uliibua pongezi kutoka kwa wengi akiwemo meneja wa Liverpool Jurgen Klopp.

"Upendo ambao nimepokea umekuwa wa kushangaza, imekuwa ya kushangaza na sijawahi kuona aina hii ya usaidizi," Lokonga alisema katika mahojiano.

"Kwangu mimi, nilikuwa na mazungumzo na Arsenal na hitimisho lilikuwa jambo bora kwangu ilikuwa kuondoka klabu. Sasa ni juu ya wakala wangu na klabu kutafuta kitu. Bado nina mkataba huko, mwaka mmoja pamoja na chaguo la mwaka mmoja tuone nini kitatokea."

Vilabu kadhaa vya Ulaya tayari vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Lokonga, ambaye atakaa mapumzikoni wiki chache zijazo kabla ya kufanya uamuzi kuhusu timu yake ijayo. Wakati huo huo, mkufunzi wa Gunners Mikel Arteta anatarajiwa kuidhinisha mauzo ya fowadi Eddie Naketiah msimu huu wa joto.

Nketiah ametatizika kupata muda wa kucheza msimu huu na atakuwa mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa kuondoka katika wiki zijazo. Mohamed Elneny na Cedric Soares pia wataondoka katika klabu hiyo, huku Aaron Ramsdale akionyesha ari ya kuondoka pia.

View Comments