In Summary

•Kiungo wa kati wa Ubelgiji,Romeo Lavia ameelezea ubingwa alionao kocha mteuzi wa chelsea,Enzo Maresca.

•Enzo Maresca amefanya kazi pamoja na Romeo Lavia na Cole Palmer akiwa Manchester  City kama msaidizi wa Pep Guardiola mwaka wa 2021.

Romeo Lavia
Image: CHELSEA

Enzo Maresca aliteuliwa kama kocha mkuu wa Chelsea na atakutana na baadhi ya sura anazozijua kama vile Romeo Lavia na Cole Palmer,baada ya kuwa nao Manchester City,2021.

Romeo  Lavia,kiungo wa kati kutoka Ubelgiji ametoa ufahamu wa jinsi muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 44 anavyofanya kazi baada ya kuhamia jijini London.

Lavia amecheza dakika 20 pekee chini ya meneja wa zamani Mauricio Pochettino huku majeraha yakimkosesha muda wa kucheza,baada ya kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 53 kutoka Southampton msimu uliopita wa joto

Kiungo huyo alizungumzia uwezo wa Maresca mwaka 2021, kule Manchester City akisema kuwa alifurahia kufanya kazi na meneja huyo na akaeleza jinsi uchezaji wake na uwezo wa kukuza wachezaji wachanga umekuwa ufunguo wa maisha yake ya ukocha.

“Ninafurahia sana kurejesha mpira na kupita kwenye mistari. Maresca  alinisaidia sana kwa hilo, kila mara nikiwa kwenye zamu ili niweze kuona mchezo unasonga mbele, kwa hivyo sio shida sasa...Najua kwamba nina sifa zangu, lakini nikifanya kitu kibaya wananisaidia. Ni wazi, wachezaji wenzangu wana uzoefu - baadhi yao wamefanya mazoezi na kikosi cha kwanza. Wamenisaidia sana na nitaendelea kujifunza."

Chelsea ilimaliza msimu katika nafasi ya sita chini ya Mauricio Pochettino, na kushinda mechi zao zote tano zilizopita lakini hiyo haikutosha kuokoa kazi yake kwani kukosa kucheza ligi ya mabingwa na kutokubaliana juu ya uhamisho kulimfanya muargentina huyo kuachishwa kazi.

 

View Comments