In Summary

•Mwenyekiti wa Gor Mahia ametakiwa kufika mahakamani kujitetea kwa kukosa kulipa kocha wa zamani wa Gor Mahia Francis Nuttal.

•Francis  Nuttal alikinoa kikosi cha Gor Mahia 2024 na 2016 huku akishinda taji mwaka wa 2015.

Mwenyekiti wa Gor Mahia ;Ambrose Rachier
Image: Gor Mahia

Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier ametakiwa kufika mbele ya mahakama ya ajira na uhusiano wa kazi jijini Nairobi kwa  kukosa kumlipa fidia ya kuachishwa kazi kocha wa zamani wa Kogalo,Francis Nuttall.

Rachier atalazimika kufika mbele ya mahakama mnamo Julai 18,2024 saa tatu asubuhi ili kuonyesha sababu za kutofungwa jela kwa kukosa kumlipa kocha wa zamani wa Gor Mahia,Francis Nuttal;fidia ya kuachishwa kazi kimakosa kulingana na maamuzi ya mahakama.

Francis Nuttal alikinoa kikosi cha Gor Mahia kati ya 2014 na 2016 huku akishinda taji la 2015 bila kushindwa kwa mechi yoyote.Kocha huyo amechukua hatua za kisheria dhidi ya Gor Mahia akitaka kulipwa fidia kwa kutimuliwa kinyume cha sheria.

Kulingana na Mozzart Sport, Nuttall alidai kwamba mnamo Novemba 2015, kilabu hio  ilijaribu kubadilisha mkataba wake kwa kupendekeza kukatwa kwa 50% badala ya nyongeza ya 10% ya mwaka iliyoainishwa katika mkataba wake.

Mkongwe huyo aidha  alitaka  kutunukiwa  posho ya nyumba ambayo haijalipwa,Ksh.1,440,000 posho ya gari Ksh.3,360,000 tikiti za ndege kwa ajili yake na familia yake ,Ksh.810 ,000+Ksh.3,195,489 , bima ya matibabu,mshahara badala ya Ksh.770,000 pamoja na na kompyuta ya mkononi Ksh.100,000.

Katika hukumu iliyotolewa Machi 20,2023 na jaji B.O.M Manani,Nuttal alitunukiwa Ksh.2,800,000 kwa kukatisha mkataba wake isivyostahili,sawa na mshahara wa jumla wa miezi minne.

Hukumu hii ilithibitishwa baadaye Machi 20 mwaka huu. Licha ya hayo miezi mitatu imepita bila klabu hiyo kutii amri ya mahakama hivo kusababisha kuitwa tena.

View Comments