In Summary

• Southgate aliliambia gazeti la Ujerumani Bild,kwamba kukosa kombe nchini Ujerumani kunaweza kumfanya kuondoka .

Image: BBC

Meneja Gareth Southgate anasema Euro 2024 inaweza kuwa "nafasi yake ya mwisho" kushinda kombe akiwa na England.

Mchezaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 53 amekuwa kocha tangu 2016, akiipeleka timu yake nusu fainali ya Kombe la Dunia 2018, fainali ya Euro 2020 na robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Mkataba wake unatarajiwa kumalizika Disemba lakini Chama cha Soka kinatamani abaki kama meneja wa Kombe lijalo la Dunia mwaka 2026 nchini Marekani, Canada na Mexico.

Hata hivyo, Southgate aliliambia gazeti la Ujerumani Bild,kwamba kukosa kombe nchini Ujerumani kunaweza kumfanya kuondoka .

"Ikiwa hatutashinda, labda sitakuwa hapa tena. Basi inaweza kuwa nafasi ya mwisho," alisema.

"Ikiwa tunataka kuwa timu kubwa na ninataka kuwa kocha wa juu, basi lazima tufanye kazi ya ziada namuhimu."

Maandalizi ya kikosi cha Southgate kwa mchuano huo yamekuwa na mseto wa kusajiliushindi wa 3-0 dhidi ya Bosnia-Herzegovina na kufuatiwa na kichapo cha kusikitisha cha 1-0 kutoka kwa Iceland siku ya Ijumaa.

Uingereza itaanza kampeni yake ya Euro dhidi ya Serbia mjini Gelsenkirchen Jumapili, 16 Juni kabla ya mechi dhidi ya Denmark na Slovenia.

"Nafikiri takriban nusu ya makocha wa kitaifa wanaondoka baada ya michuano - hiyo ndiyo hali ya soka ya kimataifa," alisema Southgate, ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United ikiwa watamtimua Erik ten Hag .

"Nimekuwa hapa kwa karibu miaka minane sasa na tumekaribia. Kwa hivyo najua kwamba huwezi kuendelea kusimama mbele ya umma na kusema 'tafadhali fanya zaidi kidogo', kwa sababu wakati fulani watu watapoteza imani na ujumbe wako.

View Comments