In Summary

•De la Fuente amekitaja kikosi cha Italia kuwa na nguvu na ubora kabla ya pambano la leo ,Juni 20 kwenye mashindano ya Euro 2024.

•Timu itakayoibuka na ushindi hii leo itakuwa imejikatia tiketi ya kufuzu raundi ya kumi na sita  kwenye mashindano hayo.

De la Fuente Kocha wa Uhispania
Image: Hisani

Kocha mkuu wa Uhispania,De la Fuente amesema kuwa watafanya lolote lile ili kuibuka na ushindi kwenye mechi dhidi ya Italia ,mashindano ya Euro 2024.

Kwenye mahojiano na waandishi wa habari siku ya Jumatano,De la Fuente amesema kuwa anafahamu mchezo wa Italia na atafanya chochote kuwasimamisha.

"Mabingwa watetezi Italia  walishinda mechi yao ya ufunguzi ya Euro 2024 dhidi ya Albania kwa mtindo wa kushambulia bila kutarajiwa, lakini Uhispania wapinzani wao siku ya Alhamisi hawajafadhaika..." Meneja Luis de la Fuente alisema.

Aliweka wazi kuwa timu yake haijiandai kwa mchezo wa kushambulia , hata hivyo alisema kuwa anafahamu Italia watajaribu kumiliki asilimia kubwa ya mchezo.

Aliongeza,

"Tunajua wanacheza soka ya aina gani na wana ushindani kiasi gani, kwa hivyo hatutashangaa. Natarajia Italia yenye nguvu na ukali ambayo itajaribu kudhibiti kumiliki mpira. Ni mechi muhimu zaidi katika hatua ya makundi."

Baada ya kuicharaza Croatia mabao 3-0, Uhispania wanaongoza Kundi B huku Italia wakishilkilia nafasi ya pili.Ikiwa timu moja itaibuka na ushindi leo Alhamisi basi itakuwa imejikatia tiketi kwa hatua ya 16.

Croatia na Albania wako mkiani wakiwa na pointi moja baada ya kutoka sare ya 2-2 siku ya Jumatano.

Miamba hao wawili wanakutana kwa mara ya nane tangu mwaka wa 1960.Huku wakijiandaa kumenyana katika makala ya tano mfululizo, De la Fuente alikiri kuwa timu yake pia inacheza soka vitofauti na matarajio ya mashabiki.

Je,ni nani ataibuka na ushindi hii leo Juni 20 kwenye pambano hilo kali?

View Comments