In Summary

•Messi amempita Sergio Livingstone wa Chile ambaye alicheza mechi 34 kwenye mashindano ya Copa America.

•Argentina walionyesha ubabe wao baada ya kuwarindima Canada  2-0 kwenye mashindano ya Copa  America.

Lionel Messi
Image: INSTAGRAM

Mshambulizi wa Argentina ,Lionel Messi ameweka rekodi mpya ya kucheza Copa America kwa wingi,35 kuliko mchezaji yoyote yule.

Mchezaji huyo wa Intermiami alianza kwenye mechi kati ya  Argentina na Canada  katika ushindi wa  Argentina wa mabao 2-0  Ijumaa asubuhi.

Messi  alimpita Sergio Livingstone wa Chile akiwa amecheza mechi 34 na kutinga kwenye kikosi cha kwanza cha Lionel Scaloni mjini Atlanta. Zizinho wa Brazil amecheza mechi 33 na Víctor Agustín Ugarte 30 wa Bolívia  anafunga nne bora.

Messi, ambaye anatimiza umri wa miaka 37 Jumatatu ,pia aliendeleza rekodi yake ya Copa América ya kutoa pasi za mabao kwa bao lake la 18 baada ya kuunganisha pasi iliyojaa uzani kwa Lautaro Martínez, aliyefunga bao la pili la Argentina.

"Tulijua utakuwa mchezo mgumu. Kwa bahati nzuri tulipata bao mapema katika kipindi cha pili, lakini Canada bado waliweza kufanya mchezo kuwa mgumu kwetu," Messi alisema baada ya mchezo huo.

Aliongeza ;"Wapinzani wengi wanacheza tofauti dhidi yetu. Muhimu wetu ni kuwa na subira na kuhamisha mpira kutoka upande hadi mwingine."

Fowadi huyo alicheza kwa mara ya kwanza katika mashindano ya Conmebol mwaka wa 2007, akianza mechi dhidi ya Venezuela chini ya meneja wa zamani wa Argentina Alfio Basile. Messi aliendelea kushiriki katika mechi sita za La Albicelete mwaka wa 2007, ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa mabao 3-0 na Brazil.

Tangu wakati huo, Messi amecheza katika matoleo ya 2011, '15,'16, '19,'21 na '24 ya Copa América na kufikisha jumla ya mechi 35. Argentina walishinda taji hilo miaka mitatu iliyopita na kufikisha jumla ya ushindi wa Copa hadi 15, lakini ilikuwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo wakati wa Messi.

Mshambulizi huyo mashuhuri pia hivi karibuni anaweza kuvunja rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye Copa América. Kwa sasa anashikilia nafasi ya 13 katika michezo 35.

Ubingwa katika Copa América utaifanya Argentina kuwa timu ya kwanza katika historia ya Amerika Kusini kupata mataji matatu ya mashindano makubwa mfululizo, baada ya kushinda toleo la 2021 na kombe la dunia la 2022.

Uhispania ndio timu pekee iliyofanikiwa kupata ushindi huo baada ya kushinda ubingwa wa kombe la bara  mnamo 2008 na 2012, na pia kombe la dunia la 2010.

View Comments