In Summary

• Ligi ya FKF Premier League ilikamilika Jumapili ya Juni 23 na police FC walimaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Gor Mahia na Tusker FC.

Basi jipya la Police FC.
Image: FACEBOOK// POLICE FC

Klabu ya Police FC inayoshiriki ligi kuu ya FKF-PL humu nchini wamezindua basi jipya maridadi kwa ajili ya shughuli za usafiri kwa wanabunduki hao.

Kupitia ukurasa wao wa Facebook, Police FC walipakia msururu wa picha na video wakionyesha maboresho makubwa ya usafiri wao, kutoka kwa kutumia basi la zamani kuukuu hadi kupata basi jipya lenye maboresho ya kisasa.

“Dhahabu Hata ififie Haiwezi Kua Shaba #BabaYao. Kizuri ni kizuri Tu!!” waliandika kwenye msururu wa picha hizo.

Police FC inakuwa timu nyingine humu nchini kumiliki basi la kisasa kwa ajili ya usafiri wa wachezaji baada ya AFC Leopards, Tusker FC, FC Talanta na Gor Mahia.

Gor Mahia walikabidhiwa basi lao la kifahari mwaka jana kutoka kwa wakfu wa Eliud Owalo Foundation.

Ligi ya FKF Premier League ilikamilika Jumapili ya Juni 23 na police FC walimaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Gor Mahia na Tusker FC.

Mapokezi ya basi kwa Police FC yanakuja siku chache baada ya PS wa wizara ya usalama wa ndani Raymond Omollo kutoa ahadi ya kuipa timu hiyo basi la kisasa.

View Comments