In Summary

• Alianza kucheza Ligi ya Premia Januari 2023 akiwa na umri wa miaka 17, na akafanikiwa tu msimu wa 2023-24 akiwa na klabu yake.

• Mainoo alikua mchezaji mdogo zaidi wa England kucheza nusu fainali ya mashindano makubwa na alionyesha kwa nini Southgate ameweka imani yake kwake.

KOBBIE MAINOO

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amekiri kwamba kikosi chake hakikuwahi kupata mchezaji wa kudhibiti kiungo cha kati kama kinda Kobbie Mainoo kwa muda mrefu sasa.

Mainoo alikuwa mmoja wa wachezaji walioleta tofauti kubwa uwanjani wakati wa pambano la nusu fainali bali ya Uingereza na Uholanzi.

Katika mechi hiyo, Uingereza walitoka nyuma na kuchukua ushindi wa 2-1 dakika za mwisho na kujikatia tikiti ya kuingia kwenye fainali ambayo itachezwa Jumapili dhidi ya Uhispania ambao waliwabandua Ufaransa siku mbili zilizopita.

Alianza kucheza Ligi ya Premia Januari 2023 akiwa na umri wa miaka 17, na akafanikiwa tu msimu wa 2023-24 akiwa na klabu yake.

Mainoo alikua mchezaji mdogo zaidi wa England kucheza nusu fainali ya mashindano makubwa na alionyesha kwa nini Southgate ameweka imani yake kwake.

"Nadhani uchezaji wake wote umekuwa wa kipekee, haswa unapozingatia umri wake," Southgate aliwaambia wanahabari.

"Hatujapata mchezaji kama yeye hadi sasa. Inaleta tofauti kubwa wakati wachezaji wako wa safu ya kati wanaweza kupokea mpira wakiwa wanabanwa, kugeuka na mpira kwa urahisi na kwa raha na hata kutoa pasi.

"Nilimfikiria, Phil (Foden) akitokea kwenye nafasi, Jude (Bellingham), mwendo wetu ulikuwa mzuri sana. Ilisababisha matatizo mengi na wao kuzoea bila mpira."

Kiungo huyo wa kati wa Manchester United aliiweka Uholanzi ndani kabisa ya himaya yao kwa kuweka shinikizo kubwa kwenye mpira kila walipojaribu kuuruka.

View Comments