In Summary

•Chelsea wametoa jezi zao mpya bila mfadhili wa mbele baada ya kushindwa kupata makubaliano mapya kabla ya tarehe ya mwisho ya utengenezaji.

•Kieranan Dewsburry-Hall atavalia jezi namba 22 aliyoipendelea akiwa Leicester City.

Jezi mpya ya Chelsea 2024/25
Image: Chelsea football club

Chelsea wamezindua jezi yao mpya ya nyumbani kwa msimu wa 2024/25, huku mashabiki wengi wakionekana kutofurahishwa na muundo huo.

Chini ya kaulimbiu 'We Burn Blue', jezi mpya ya Chelsea inawapa msukumo wachezaji pamoja na mashabiki  na  kuunganisha klabu nzima nyuma ya nia ya pamoja ya kufanikiwa ndani na nje ya uwanja.

Kwa mara nyingine, Chelsea wametoa jezi zao mpya bila mfadhili wa mbele baada ya kushindwa kupata makubaliano mapya kabla ya tarehe ya mwisho ya utengenezaji.

Mkataba wa awali wa The Blues na Infinite Athlete ulikuwa mkataba wa mwaka mmoja kwani Chelsea walikuwa wameweka dau la kurejea Ligi ya Mabingwa msimu huu na kuweza kufanya mazungumzo ya kupata udhamini bora zaidi.

Infinite Athlete wamehamia  kwenye  jezi za mazoezi za Chelsea lakini utafutaji wa mbadala kwenye sehemu ya mbele ya jezi zao mpya unaendelea.

Hata hivyo,mabadiliko ya  nambari kwenye jezi yalithibitishwa;

Tosin Adarabioyo atavaa jezi 4 ambayo haijavaliwa tangu Benoti Badiashile msimu wa 2022/23, huku mchezaji mwenzake mpya Kiernan Dewsbury-Hall akishika namba 22 aliyoipendelea wakati akiwa na Leicester City. Hakim Ziyech alikuwa mchezaji wa mwisho kuvaa jezi hiyo kwa Chelsea.

Omari Kellyman amekabidhiwa 37, Marc Guiu anachukua 38  huku  Renato Veiga  akichukua jezi namba 40.

Moja ya mabadiliko makubwa ni kubadili kwa Levi Colwill. Beki huyo wa kati alivaa 26 msimu uliopita lakini sasa amehamia kutwaa jezi 6 ambayo iliachwa nyuma na Thiago Silva. Wesley Fofana pia amepanda kutoka 33 hadi 29.

View Comments