In Summary

•Wasiwasi imetanda miongoni mwa mashabiki wa Manchester United baada ya beki Yoro kuonekana akitembea kwa kutumia mikongojo.

•Vyanzo tofauti vinaripoti kuwa Manchester United bado wapo sokoni kumtafuta beki mpya,Matthijs de Ligt  wa Bayern Munich akipigiwa upatu.

Leny Yoro Beki wa Manchester United
Image: Instagram/ESPN

Sajili mpya wa Manchester United , Leny Yoro huenda  ikamchukua muda mrefu kupona jeraha baada ya kuonekana akitembea kwa kutumia mikongojo. 

Yoro,aliyesajiliwa kwa pauni milioni 59  alitolewa  katika dakika ya 33  kwenye mechi ya Manchester United dhidi ya Arsenal,waliopoteza 2-1.

Picha  zake akitumia magongo na kuvaa kiatu cha plastiki kwenye mguu wake wa kushoto katika UCLA, kituo cha mazoezi cha United huko LA zimekuwa zikisambaa mtandaoni.

Huenda  bingwa huyo atakuwa nje kwa muda mrefu,na itakuwa  pigo kubwa kwa United na mkufunzi Erik ten Hag, ambaye alipanga kuanza msimu mpya huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 akiwa kiini cha safu yake ya ulinzi.

Mipango ya mkufunzi Eric Ten Hag ilikuwa ni kumujuisha beki Leny Yoro kwenye timu ya kwanza hasa baada ya Varane kuondoka msimu jana.

Varane amejiunga na Como ya Italia baada ya kuondoka Old Trafford kwa uhamisho wa bure mwishoni mwa msimu uliopita.

Vyanzo mbali mbali  vinaripoti kuwa   United bado wako sokoni kutafuta beki mwingine wa kati na wana nia ya kuwanunua Matthijs de Ligt wa Bayern Munich na Jarrad Branthwaite wa Everton.

Bayern wanataka £42m kwa De Ligt huku Everton wamenukuu zaidi ya £70m kwa Branthwaite.

United tayari wametuma ofa mbili rasmi kwa Branthwaite, ambazo zote zimekataliwa na Everton.

United pia wana wasiwasi kuhusu mshambuliaji Rasmus Højlund, ambaye alitolewa katika kipindi cha kwanza dhidi ya Arsenal baada ya kupata jeraha linaloshukiwa kuwa la msuli wa paja.

View Comments