logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Highway yailemea Musinga kwenye fainali licha ya kucheza na wachezaji 10

Katika kitengo cha wasichana, Butere Girls ilifanikiwa kutetea taji lao kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Nyakach.

image
na Davis Ojiambo

Michezo08 August 2024 - 13:59

Muhtasari


  • • Katika kitengo cha wasichana, Butere Girls ilifanikiwa kutetea taji lao kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Nyakach.
Mechi za shule za upili

Shule ya Sekondari ya Highway imeweka historia kwa kuwa Bingwa mpya wa Kitaifa baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2 kwenye mikwaju ya penalti dhidi ya Musingu kwenye Uwanja wa Gusii.

Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 1-1 baada ya muda wa kawaida, shukrani kwa mabao ya mapema kutoka kwa timu zote mbili. 

People Daily wanripoti kuwa Elvis Ochieng alitangulia kuifungia Highway dakika ya 14 tu ya mchezo kwa juhudi za karibu, na kuwafanya kuongoza 1-0.

Hata hivyo, Musingu walisawazisha haraka dakika tano baadaye Alvin Oloo alipoachia shuti kali la mbali.

Licha ya kupunguzwa hadi wachezaji kumi baada ya kadi nyekundu, Highway ilishikilia msimamo, na kulazimisha mechi kuelekea mikwaju ya penalti.

Katika mikwaju ya penalti, Musingu walipoteza penalti yao ya kwanza baada ya mkwaju kupanguliwa na mlinda lango wa Highway.

Baada ya mkwaju wa mwisho wa Musingu kuoolewa, ulihitimisha taji la Shule ya Sekondari ya Highway.

Katika kitengo cha wasichana, Butere Girls ilifanikiwa kutetea taji lao kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Nyakach.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved