Kocha wa klabu ya Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza Pep Guardiola amesema kuwa Rico Lewis ni mchezaji bora.
Kinda huyo nayecheza kama kiungo mkabaji alitokea akademia ya timu hiyo na kuwa kiungo muhimu huku akivalia jezi nambari 82.
Baada ya timu ya City kuilabua Chelsea mabao mawili kavu, katika mechi ya ufunguzi,Pep alimsifia sana Lewis akisema amependezwa namna alicheza katika safu ya ulinzi .
Aidha ,Lewis ni mchezaji mwenye uzoefu katika nafasi ya ulinzi pande zote mbili ,na ambaye aliiongoza timu ya Manchester city U18 akiwa na umri wa miaka 15 kuonyesha umahiri katika taaluma ya kusakata soka huku wakishinda taji hilo 2018.
Msimu wa 2022-23, Lewis alijumuishwa katika kikosi cha kwanza timu ya City na ambapo alianzishwa katika timu ya kwanza na kupachipika bao walipokuwa wakicheza na Sevilla katika kombe la maskio marefu.
Lewis, ambaye alitia mkataba wake wa miaka mitano mwaka jana amekuwa na ubora wake akiichezea timu hiyo ya City ambapo wameshinda mataji ikiwemo kombe kuu la ligi ya Uingereza mara nne mfululizo.
Kando na timu ya City ,Lewis ameichezea timu ya taifa ya Uingereza U18 na kucheka na wavu mara moja.Lewis amefunga mabao 3 katika taaluma yake.