logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fulham yakubaliana na Burnley kumsajili Sander Berge

Marco Silva aamua kuimarisha kikosi cha timu ya Fulham Unuted ili kuweka upinzani mkali msimu huu.

image
na Davis Ojiambo

Michezo20 August 2024 - 11:42

Muhtasari


  • •Tim ya Fulham United ,yakubaliana na klabu ya Burnley ili kumsajili kiungo mkabaji mzawa wa Norway,kwa kima cha £25m ili kujinga timu hiyo ambayo ilimaliza katika nafasi ya 10 msimu jana.
SANDER BERGE

Timu ya Fulham inayoshiriki katika ligi kuu nchni Uingereza sasa imeboresha mazungumzo na klabu ya Burnley inayoshiriki ligi ya daraja la pili ligi humo kuhusu swala la kumsajili kuingo mkabaji wa timu hiyo Sanda Berge baada ya mkataba wake na klabu hiyo ya Burnley kutamakita.

Timu ya Fulham ambayo ilimaliza katika nafasi ya 10 na alama 52 katika msimu jana.Fulham wameonyesha uwezo wa kumsajili kiungo huyo kwa kima cha £25m ili kujiunga na timu hiyo ili kuboresha safu ya ulinzi na vile vile utafutaji mabao .

Berge ,alianzisha taaluma yake kama mchezaji katika klabu ya Asker .Aidha ,Berge alicheza katika kombe la masikio Champions League na klabu ya RB Salzburg na kuzidi ,kuimarika zaidi.

Mreno Marco Silva ,ambaye ni kocha mkuu wa Fulham ,ameonyesha kujituma hasa katika kukipanga kikosi ambacho ni hodari ili kuwania mataji katika shirikisho  la Uingereza.

Fulham United, ilipigwa bao moja kavu na timu ya ManchesterUnited katika mechi ya ufunguzi wakiwa ugenini .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved