logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mshambuliaji wa Chelsea, Armando Broja kuelekea Ipswich Town kwa mkopo

Ipswich watatakiwa kufanya uhamisho wake wa mkopo kuwa uhamisho wa kudumu kwa pauni milioni 30.

image
na Davis Ojiambo

Michezo21 August 2024 - 09:58

Muhtasari


  • • Ujio wa kocha mpya, Enzo Maresca umeonyesha dalili kwamba mchezaji huyo hana lake tena katika kikosi cha Chelsea msimu huu na chaguo bora kwake ni kukipipiga kibarua chake kwingine.
ARMANDO BROJA

Timu ya Ipswich Town,iliyopandishwa ngazi msimu huu ,imekubaliana na klabu ya Chelsea kumchukua mshambuliaji Armando Broja, ambaye atajiunga na klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mzima.

Aidha Chelsea,wameiambia timu ya Ipswich, kwamba ni lazima wamsajili Broja kwa mkataba wa kudumu endapo atawasaidia kutoshushwa daraja mwishoni mwa msimu huu,kwa kima cha £30m.

Ipswich ilimaliza katika nafasi ya pili katika ligi ya daraja la pili kwa alama 96 ,sasa wako kwenye mchakato wa kuwania ligi licha ya kuchabangwa mabao mawili kavu na timu ya Liverpool katika uga wa nyumbani.

Armando Broja amekuwa mchezaji mwiba hasa kutafuta mabao pale The Blues lakini hajaweza kupata nafasi ya kucheza katika michuano mingi.

Ujio wa kocha mpya, Enzo Maresca umeonyesha dalili kwamba mchezaji huyo hana lake tena katika kikosi cha Chelsea msimu huu na chaguo bora kwake ni kukipipiga kibarua chake kwingine.

Broja ambaye alizaliwa Uingereza ,lakini anaitumikia timu ya taifa ya Albania, anauzoefu baada yakuwa amejumuishwa katika klabu hiyo na kupata tajiriba .Kinda huyo ambaye alitokea klabu ya BurnHam, amezichezea klabu za FulHam united na Southampton kwa mkopo na kuchangia pakubwa katika timu hizo.

Kuondoka kwake pale Chelsea kumechamngiwa pakubwa mna sajili ambazo timu hiyo inafanya, na kwaivyo kukosa nafasi.

Broja anatarajiwa kutamatisha vipimo vyake vya kiafya kabla ya leo,katika timu hiyo chini ya mkufunzi Kieran Mckenna ambaye aliwaziwa kuchukua pengo lake Pochettino.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved