logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Tore Bobe!” SportPesa kuwa mdhamini mpya wa Shabana FC

Kupitia X, Shabana walinukuu ujumbe wa SportPesa kuwakaribisha na kusema, “Hapa ndipo.”

image
na Davis Ojiambo

Michezo22 August 2024 - 08:54

Muhtasari


  • • “Tore Bobe, karibu kwenye nyumba yako mpya!!🤝 Imethibitishwa, Imetiwa Saini na Kufungwa,” SportPesa waliandika kwenye ukurasa wao wa Facebook.
SHABANA FC

Klabu ya Shabana FC inayoshiriki katika ligi kuu ya FKF-PL nchini Kenya imeripotiwa kupata mfadhili mpya kwa kampeni ya msimu huu wa mwaka 2024/25.

Kupitia ukurasa wao wa X, Shabana, licha ya kutotoa tangazo rasmi kuhusu ufadhili huo, walionekana wakiwajibu mashabiki waliokuwa wakihoji kuhusu jezi mpya za mfadhili huyo.

Uvumi wa kupata mfadhili mpya ulizuka baada ya kampuni ya Kamari ya SportPesa kuchapisha ujumbe wa kuwakaribisha Shabana kama washirika wapya katika kutangaza chapa yao katika soka.

“Tore Bobe, karibu kwenye nyumba yako mpya!!🤝 Imethibitishwa, Imetiwa Saini na Kufungwa,” SportPesa waliandika kwenye ukurasa wao wa Facebook.

Kupitia X, Shabana walinukuu ujumbe wa SportPesa kuwakaribisha na kusema, “Hapa ndipo.”

Kuhusu suala la Jezi, Shabana walisema kwamba ndio wako katika hatua za lala salama kuchapisha jezi zenye chapa ya SportPesa na pia kuzisafirisha katika maduka rasmi kwa ajili ya kununuliwa na mashabiki.

“Ikiisha tutawasiliana kwa uhakika, tunakamilisha uzalishaji na usafirishaji,” Shabana walijibu.

Itakumbukwa klabu hiyo kutoka eneo la Gusii yenye ushabiki mkubwa ilirudi kwenye ligi msimu uliopita baada ya kuwa nje kwa miaka 17.

Shabana walikuwa wanafadhiliwa na kampuni nyingine ya Kamari, Bang Bet – mfadhili ambaye walimpata msimu jana ukianza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved