Kinda Endrick Felipe Moreira de Sousa ambaye ni mzaliwa wa Brazil ,mwenye umriwa miaka 18 ambaye anachezea timu ya Real Madrid kwenye ligi kuu ya Uhispania, La Liga sasa ndiye mchezaji mdogo zaidi kutoka nche ya Uhispania kuwahi kuifungia timu hiyo.
Endrick, na ambaye pia huchezea timu ya taifa ya Brazil, alifunga bao siku ya Jumapili wakati timu ya Real Madrid ilikuwa inacheza na timu ya Valladolid alipoingia kama nguvu mpya kunako dakika ya 86 na kupata bao.
Mshambulizi huyo, alianza soka lake na kujulikana na wengi akiichezea timu ya Palmeiras akiwa na umri wa miaka 11 na kuchangia magoli mengi klabuni humo hadi alipoondoka.
Aidha, Endrick ndiye mchezaji mdogo zaidi kuwahi kujumuishwa katika kikosi cha taifa baada Ronaldo mwaka jana katika mashindano ya kutafuta tiketi ya kucheza katika kombe la Dunia mwaka jana.
Endrick alisajiliwa na klabu ya Real Madrid kutoka Palmeiras na mechi ya Jumapili imekuwa mechi yake rasmi katika ligi hiyo .
Endrick anarajiwa kutamba katika klabu ya mashabiki wa klabu hiyo kutokana na mchezo wake wa haiba licha ya umri wake mdogo.Endrick ambaye ameiga nyayo zake mchezaji wa timu hiyo wa zamani Christiano Ronaldo kutoka Ureno.