In Summary

•Katika mahojiano hayo, alizungumzia mafanikio ambayo mashetani wekundu wameyapata katika misimu miwili iliyopita.

•Alieleza imani yake na wachezaji wake, akipuuza madai kwamba wanakosa kufanya kile alichowaombia kwenye mazoezi.

Image: HISANI

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag amesisitiza kuhusu azma ya timu yake kushinda mataji msimu huu licha ya kuanza vibaya.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 54 alifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi ya United dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Old Trafford siku ya Jumapili jioni ambapo alizungumza kuhusu imani yake na timu hiyo.

Katika mahojiano hayo, alizungumzia mafanikio mbalimbali ambayo mashetani wekundu wameyapata katika misimu miwili iliyopita ambayo amekuwa akiwanoa na kubainisha kuwa timu hiyo bado itafanikiwa kutwaa mataji zaidi msimu huu.

"Katika miaka miwili, tulichukua mataji mawili. Mwisho wa msimu utaona tutakapokuwa,” ten Hag alisema.

Aliongeza, “Najua tutakuwa wapi mwisho wa msimu. Tutakwenda kuchukua mataji.”

Meneja huyo raia wa Uholanzi alieleza imani yake na wachezaji wake, akipuuza madai kwamba wanakosa kufanya kile alichowaombia kwenye mazoezi.

Jumapili jioni, mashetani wekundu walipata kichapo cha aibu kutoka kwa wapinzani wao wa muda mrefu, Liverpool wakiwa nyumbani Old Trafford.

Ten hag hawakuweza kufunga hata bao moja wakati Liverpool wakifunga mabao matatu dhidi ya mlinda lango Andre Onana.

Luis Diaz aliifungia The Reds mabao mawili, huku Mohamed Salah akifunga bao moja na kujinyakulia ushindi wa 0-3 dhidi ya United katika mchezo huo wa kusisimua.

View Comments