In Summary

• Ikiwa ni wiki mpya akiwa na Ureno, Ronaldo sasa atarejea Saudi Arabia huku Al-Nassr akitarajia kupata ushindi wa pili mfululizo kwenye Ligi ya Saudia.

• Watamenyana na Al-Ahli wakati mapumziko ya kimataifa yatakapomalizika na Ronaldo anaweza kumenyana na mchezaji mpya Ivan Toney.

RONALDO.
Image: HISANI

Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes amemtabiria nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo kufikisha idadi jumla ya mabao zaidi ya 1,000 katika taaluma yake ya soka.

Hii ni baada ya Ronaldo kutokea kwenye benchi kipindi cha pili na kuifungia Ureno bao la ushindi Jumapili usiku katika mpambano kati yao ya Scotland.

Akizungumza baada ya mechi kumalizika, Fernandes alisema: “Ushawishi huwa ni uleule siku zote, bila kujali anaanza benchi au la, kila aliyeingia alifanya tofauti, Cristiano ana bao, leo amefunga bao lake la 901 na sasa yupo njia yake kwa elfu, ambayo ndiyo anayotaka."

Fernandes aliangazia ukweli kwamba Ronaldo sasa yuko njiani kufikisha mabao 1000 na licha ya nyota huyo wa soka kuwa na umri wa miaka 39, hungeweka dau dhidi yake kufika hapo kabla hajastaafu.

Ronaldo alikuwa na ushawishi mkubwa kwenye mchezo wa Scotland alipoingia uwanjani na kwa mara nyingine akathibitisha kuwa bado anaweza kuwa tofauti kwa nchi yake, baada ya kuifungia Ureno bao la ushindi dhidi ya Croatia katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mataifa ya Afrika Alhamisi na kufikisha mabao 900.

Ikiwa ni wiki mpya akiwa na Ureno, Ronaldo sasa atarejea Saudi Arabia huku Al-Nassr akitarajia kupata ushindi wa pili mfululizo kwenye Ligi ya Saudia.

Watamenyana na Al-Ahli wakati mapumziko ya kimataifa yatakapomalizika na Ronaldo anaweza kumenyana na mchezaji mpya Ivan Toney.

 

View Comments