In Summary

• Chelsea kwa mara ya pili msimu chini ya mwezi mmoja watacheza mechi wakisimamiwa na refa Anthony Taylor.

• Mashabiki wa Chelsea hawampendi Taaylor kutokana na uamuzi wake wa kushangaza.

Refa Anthony Taylor
Image: Facebook

Chelsea kwa mara nyingine tena watacheza mechi ya ligi kuu Uingereza chini ya usimamizi wa refa Antony Taylor siku ya Jumamosi watakaposafiri kucheza dhidi ya Bournemouth ugani Vitality.

Mashabiki wa Chelsea hawampendi mwamuzi huyo kwani wanaamini kuwa Taylor anachukia klabu yao na ni vigumu kwao kupata ushindi katika mechi ambayo Taylor ni refa.

Tangu kung'oa nanga kwa msimu huu, Chelsea wamecheza chini ya Taylor mechi moja dhidi ya Manchester City mchuano waliopoteza mabao mawili katika uwanja wa nyumbani.

Mechi hiyo ilizua gumzo wakati refa aliinyima Chelsea penalti baada ya mpira kumguza Mateo Kovacic mkononi. Taylor kwa mara kadhaa ameonekana akitoa uamuzi wa kushangaza dhidi ya Chelsea kinyume na anafanya katika mechi nyingine.

Kwenye mechi hiyo ya wikendi, Antony Taylor ndiye atakuwa msimamzi mkuu akisaidiwa na Gary Beswick na Adam Nunn huku afisa wa nne wa mechi akiwa Sam Allison.

Kwenye VAR atakuwepo Peter Bankes akisaidiwa na Scott Ledger.

Mashabiki wa Chelsea tayari wameonyesha kutoridhishwa na uwepo wa refa Taylor wakidai kuwa kuna jambo lisilokuwa la kawaida linaloendelea.

View Comments