In Summary

•Richard Odada kufurahishwa na matokeo baada ya kupata ushindi dhidi ya Namibia wa 2-1, na kuweka matumaini yao hai kwa kipute cha AFCON 2025.

•Engin Firat amedokeza mikakati ambayo ameweka ili kumenyana na timu ya Intomitable Lions ya Cameroon na aghalabu kupata ushindi.

RICHARD ODADA
Image: FACEBOOK

Kiungo wa timu ya taifa ya Harambee stars,Richard Odada amesimulia furaha yake baada ya timu hiyo kuzoa ushindi wakati walikuwa wakimenyana na timu ya taifa ya Namibia katika mechi za kutafuta tiketi ya kushiriki katika kipute cha AFCON mwaka 2025, Morocco.

Stars walishinda mechi hiyo kwa mabao mawili kwa moja ,huku mabao ya timu hiyo yakitiwa kimyani na wachezaji John Avire na Duke Abuya, mechi ambayo ilichewa ugani Orlando Afrika kusini.

Aidha Odada amesema ni jambo ambalo liliwapa motisha haswa ikizingatia walicheza bila nahodha wao Michael Olunga.Alisema kuwa licha ya ukosefu wa nahodha huyo hodari, walihakikisha kuwa wameshinda mechi ili kusalia na matumaini ya kucheza katika kipute hicho cha AFCON.

Kocha wa kikosi hicho Engin Firat amesema kuwa ameweka mipanga bomba  huku wakitarajiwa kumenyana na Timu ya Taifa ya Cameroon. Kwa sasa Harambee stars inaongoza kundi J kwa alama 4 sawia na timu hiyo ya Cameroon.

Firat amesifia wachezaji wake kwa ushundi wa jana licha ya kukosa vifaa na sehemu maalum ya kufanyia mazoezi. Firat pia, amesema anakosa kikosi kamili cha kucheza nacho kwani wengi wa wachezaji wa kikosi cha kwanza wana majeraha mbali mbali.

Vile vile kocha amewasifia wachezaji kwa kutambua lengo lao uwanjani na kupata ushindi muhimu akisema kufikia sasa hawajapoteza mechi licha ya kucheza ugenini na mbali na nyumbani.

Kipute hicho ambacho kinatarajiwa kuanza desemba 2025 katika taifa la Morocco,ambapo mashabiki wa Kenya wana matumaini makubwa ,huku wakitarajia timu hiyo kufuzu kwa mara ya saba baada ya kukosa mtanange makala yaliyopita 2023, baada ya kupigwa marufuku na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA,2022.

 

View Comments