In Summary

• Aston Villa wanaanza msimu wa ligi ya klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Young Boys

UNAI EMERY Kocha wa Aston Villa
Image: X//Aston Villa

Klabu ya Aston Villa itaandikisha rekodi itakapocheza kwa mara ya kwanza katika ligi ya klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Young Boys tarehe 17 Septemba mwendo wa  1:45 jioni majira ya Afrika Mashariki.

Villa walijikatia tiketi ya kushiriki mashindano hayo makubwa katika bara la Ulaya baada ya kumaliza katika nafasi ya 4 msimu uliopita wa mwaka 2023/24.

Katika mechi yao ya ufunguzi, Aston Villa wamesafiri kuelekea Uswizi kucheza dhidi ya Young Boys inayoshiriki ligi ya juu zaidi nchini humo.

Kocha wa Aston Villa Unai Emery ameelezea matumaini yake kufanya vyema katika ligi hiyo ya klabu bingwa Ulaya.

"Natumai ni wakati mzuri kwa klabu baada ya muda mrefu wa kutowai kucheza kwenye ligi ya mabingwa. Natumai tunaweza salia hapo kwa muda mrefu kwa sababu hiyo ndio changamoto yetu."  Alisema Emery.

Vile vile, kocha Unai Emery amesema kuwa kikosi chake kina motisha na atatumia ujuzi wake kama kocha kuhakikisha Aston Villa inatoa ushindani mkubwa katika mechi zao za ligi hiyo.

Katika ratiba ya ligi ya mabingwa Jumanne ya Septemba 17  Aston Villa watamenyana na Young Boys. wakati huo  huo Juventus watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya PSV. 

Mwendo wa saa nne usiku itakuwa zamu ya Real Madrid dhidi ya VfB Stuttgart, Bayern Munich dhidi ya Dinamo Zagreb, Sporting CP dhidi ya LOSC na hatimaye Inter Milan watagwaruzana na Liverpool.

 

View Comments