In Summary

•Motsepe alisema kuna mengi ya kufanywa, lakini akabainisha ana imani na rais William Ruto kutimiza ahadi yake ya kuwasilisha viwanja hivyo.

•Kisha Motsepe akaamua kuacha kutoa maoni yoyote yanayohusiana na siasa na kuzingatia kuzungumzia soka.

Rais wa CAF// Patrice Motsepe
Image: CAF//X

Kicheko kikubwa kilijaa hewani wakati wa mkutano wa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe katika hoteli ya Kempinski Villa Rosa jijini Nairobi, Kenya siku ya Jumatatu.

Hii ilikuwa baada ya Bw Motsepe kuweka wazi imani yake kwamba serikali ya Kenya itaweza kutengeneza viwanja bora vinavyofikia kiwango cha FIFA kabla ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka ujao.

Rais huyo ambaye alizuru Kenya siku Jumapili kwa ajili kukagua viwanja vinavyoendelea kujengwa na kukarabatiwa alisema kuwa kuna mengi ya kufanywa, lakini akabainisha kuwa ana imani na rais William Ruto kutimiza ahadi yake ya kuwasilisha viwanja hivyo.

“Maoni yangu ninapoondoka ni kuamini, kwa sababu ninamwamini Rais Ruto. Kuna kazi nyingi ya kufanywa, ndio. Bado kuna kazi kubwa ya kufanya lakini ninamwamini kwa sababu ni mtu wa maneno yake, na pia kwa sababu ....,” Motsepe alisema kabla ya vicheko vikubwa chumbani kumvuruga.

Kisha akaamua kuacha kutoa maoni yoyote yanayohusiana na siasa na kuzingatia kuzungumzia soka.

Motsepe alitua nchini Jumapili kwa ziara ya siku mbili na akaenda uwanjani mara moja na ziara ya ukaguzi wa Moi Stadium, Kasarani, Nyayo Stadium na Talanta City.

Aliongozwa na Waziri wa Michezo Kipchumba Murkomen, Mkurugenzi wa Michezo wa Kenya Pius Metto na Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya, Nick Mwendwa miongoni mwa wengine.

Pia walitembelea uwanja mpya wa Talanta City wenye uwezo wa kukaa watu 60,000 katika eneo la Jamuhuri, Nairobi.

Motsepe aliandamana na Waziri wa Michezo Kipchumba Murkomen na Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya Nick Mwendwa.

Wawili hao walimhakikishia kiongozi huyo mkuu wa soka barani kuwa Kenya itakutana na ratiba iliyopangwa - Desemba.

Lakini licha ya matumaini yake, Motsepe alitaka nyasi bora zaidi kwenye uwanja wa Nyayo na Kasarani, akisisitiza nyasi za kijani kibichi zilizoidhinishwa na Fifa. Anataka viwanja lisawazishwe, viwe na alama za sare na nyeupe wazi.

View Comments