In Summary

• Timu ya Starlets U17 itafanya matayarisho ya mwisho nchini Uhispania kwa siku 11 kuanzia Alhamisi 19 Septemba.

• Starlets wataanza kampeni ya Kombe la dunia dhidi ya Uingereza mnamo tarehe 18 Oktoba mwaka 2024

Kikosi cha Harambee Starlets U7 Wakishiriki mazoezi ya pamoja Septemba 6, 2024.
Image: X//Harambee Starlets

Baada ya kufanya mazoezi humu nchini kwa wiki kadhaa, sasa wachezaji wa timu ya taifa ya wanadada ya chini ya umri wa miaka 17 watasafiri mnamo Septemba 19 kuelekea nchini Uhispania kwa kambi ya mazoezi zaidi.

Timu hiyo ya kocha Mildred Cheche tayari imecheza mechi za kujipima nguvu  na timu za wanawake zinazoshiriki ligi mbali mbali za Kenya.

Wanadada hao waliingia kambini tarehe 3 Agosti kwa mazoezi ya matayarisho ya kushiriki kombe la dunia la wanawake wa chini ya umri wa miaka 17 litakaloandaliwa nchi ya Jamhuri ya Dominican  kuanzia tarehe 16 Oktoba.

Humu nchini, timu hiyo ilicheza michuano ya kujipima nguvu na timu ya Ulinzi Starlets mechi  waliyopoteza kwa mabao 3 kwa 1.

Junior Starlets walicheza pia na Kayole Starlets mechi waliyoshinda kupitia matuta ya penalti baada ya kutoka sare ya kutofungana.

Safari ya kuelekea Uhispania ilijiri baada ya aliyekuwa waziri wa michezo Ababu Namwamba kuahidin kuwa wizara ya michezo ingegharamia safari na muda wa wachezaji hao kufanya mazoezi nchini Uhispania.

Katika ratiba ya michuano ya FIFA hiyo, Junior Starlets itaanza kampeni yake dhidi ya Uingereza tarehe 18 Oktoba, kisha kumenyana na Korea Kaskazini  tarehe 20 na kumaliza mechi za kundi lao dhidi ya Mexico.

View Comments