In Summary

•Liverpool kujikomboa baada ya kichapo wikendi dhidi ya Nottingam Forest,kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya timu ya Ac Milan ugani San Siro, 17 septemba.

•Arne Slot alipata ushindi huo muhimu huku akisherekea siku yake ya kuzaliwa huku akifikia miaka 46.

IBRAHIMA KONATE GOAL CELEBRATIONS
Image: HISANI

Klabu ya Liverpool inayoshiriki katika ligi kuu nchini Uingereza imeanza juhudi za kutetea taji la mabingwa baada ya kuipiga timu inayoshiki katika ligi ya Italia Serie A, Ac Milan wakiwa ugenini katika uga wa San Siro,17, septemba.

Vijana wa Arne Slot ,katika mechi ya wikendi kwenye ligi kuu Uingereza waliweza kupoteza mchuano wao licha ya kushinda mechi zao tatu za ufunguzi,wakicheza na Nottingam Forest nyumbani na kupoteza pambano hilo bao moja sifuri.

Kabla ya mechi hiyo,nahodha wa klabu hiyo Virgil Van Dijk,alisema kuwa lazima klabu hiyo ilitakase jina lao baada ya kibano hicho.

Kwenye mechi hiyo ambayo ilikuwa imehudhuriwa na mashabiki chini ya elfu 60, Ac Milan walipata bao lao mapema kunako dakika ya tatu chini ya mguu wake Christian Pulisic mzawa wa Amerika,baadae,Liverpool waliweza kupata bao la kusawazisha kupitia kwa beki Ibrahima Konate,nahodha Virgil van Dijk kuongeza la pili na Dominik Szoboszlai kutia msumari wa mwisho na kuipa klabu hiyo ushindi wa kwanza katika hatua ya makundi makala ya msimu huu.

Baada ya mechi hiyo sasa Ac Milan huenda wakacheza na mabingwa wa ligi ya Italia Inter Milan ambao watacheza na Manchester city jumatano ya tarehe 18, septemba.Aidha,huenda wakalazimika kucheza bila mlinda lango wao nambari moja Mike maignan ambaye alipata jeraha katika mkwaruzano huo,na kulazimika kutoka  mapema kipindi cha kwanza.

Vile vile ilikuwa siku ya furaha kwake mkufunzi wa timu hiyo Arne Slot,amabye alisherekea siku yake ya kuzaliwa kwa ushindi katika uga huo.Slot alifiksha miaka 46.

Mashabiki wa klabu hiyo ya Ac milan,walionekana kutoridhishwa na matokeo hayo baada ya kuonekana kuondoka uwanjani hata kabla ya mechi kutamatika .

View Comments