In Summary

• Klabu ya Bayern Munich kutoka Ujerumani waliititiga Dinamo Zagreb ya Croatia kibano cha mabao 9-2

Ushindi mnono kwa BAYERN NA MAN UTD
Image: facebook

Usiku wa Jumanne, mechi mbalimbali za bara Ulaya zilianza rasmi huku kukishuhudiwa mvua ya mabao katika viwanja mbalimbali.

Klabu ya Bayern Munich kutoka Ujerumani waliititiga Dinamo Zagreb ya Croatia kibano cha mabao 9-2  na kuweka rekodi ya mechi iliyoshuhudia mabao mengi zaidi katika usiku huo.

Harry Kane aliongoza kwa mabao manne, zikiwemo penalti tatu, wakati Bayern Munich wakiwasambaratisha mabingwa wa Croatia, Dinamo Zagreb 9-2.

Ubabe wa Kane ulikamilishwa na mabao ya Michael Olise, ambaye alifunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, pamoja na mabao ya Raphael Guerreiro, Leroy Sane, na Leon Goretzka.

Dinamo Zagreb, wakiwa nyuma kwa mabao 3-0 hadi mapumziko, waliwapa Bayern hofu fupi baada ya Bruno Petkovic na Takuya Ogiwara kufunga bao ndani ya dakika mbili za kila mmoja baada ya mapumziko.

Hata hivyo, Bavarians walipata udhibiti tena, wakifunga mara sita zaidi na kuhitimisha ushindi wa kina.

Katika mechi nyingine ya kufuza raundi ya 16 kwenye michuano ya Carabao, Manchester United waliwabamiza wenzao Barnsley mabao 7-0 katika uwanja wa Old Trafford.

Marcus Rashford wa Manchester United, Alejandro Garnacho na Christian Eriksen wote walifunga mabao mawili huku timu hiyo ya Old Trafford ikitinga hatua ya 16 bora.

United ilijumuishwa katika raundi ya nne na timu nyingine za Ligi Kuu ya Uingereza, Brentford, ambao waliilaza Leyton Orient ya daraja la tatu 3-1, na Crystal Palace baada ya kuwalaza Queen's Park Rangers 2-1.

Fulham walifurushwa kwa mtindo wa ajabu na wa daraja la pili Preston North End baada ya mechi kuisha 1-1 -- wenyeji wakishinda 16-15 katika mikwaju ya penalti 34, ambayo ni ndefu zaidi kuwahi katika shindano hilo.

View Comments