In Summary

• “Wakati nitafunga hattrick, nitasherehekea na ‘siuuu’ ya Ronaldo tena,” Jackson alisema.

JACKSON NA RONALDO.
Image: HISANI

Mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Senegal, niclas Jackson ameweka wazi malengo yake kwenda mbele na jinsi atakuwa akisherehekea pindi anapofunga bao.

Katika mazungumzo na wapiga picha wa Chelsea mapema wiki hii baada ya kuongeza mkataba mpya utakaomweka Stamford Bridge hadi mwaka 2033, Jackson alisema kwamba mashabiki wa Chelsea watarajie kumuona Jackson aliyeimarika kwa viwango vikubwa msimu huu.

Mshambuliaji huyo ambaye tangu kujiunga na Chelsea mwaka mmoja uliopita amekuwa akishtumiwa kwa kukosa nafasi za wazi, alisema kwamba msimu huu atakuwa anafunga mabao mengi na kila hatrrick atakayoifunga, atakuwa anasherehekea kama gwiji wa Ureno na Al Nassr, Cristiano Ronaldo.

“Wakati nitafunga hattrick, nitasherehekea na ‘siuuu’ ya Ronaldo tena,” Jackson alisema.

Ikumbukwe mchezaji huyo msimu jana alisherehekea kama Ronslo kwa kutumia staili yake ya siuu baada ya kufunga mabao matatu katika mechi yao dhidi ya watani kutoka London kaskazini, Tottenham Hotspurs.

Chelsea ilishinda mechi hiyo ugenini kwa kuinyuka Spurs mabao 4-1.

Licha ya kupoteza nafasi nyingi za wazi, Jackson amefanikiwa kufunga mabao 19 katika mechi 49 ambazo ameichezea Chelsea.

 

View Comments