In Summary

• Bayern Munich iliicharaza Dinamo Zagreb mabao 9 katika mechi ya kwanza ya klabu bingwa barani Ulaya msimu 2024/2025

Image: TWITTER// BAYERN MUNICH

Kocha wa Bayern Munich ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Manchester City Vincent Kompany amewasuta mashabiki na washikadau wa soka waliosema hawezi kuifunza timu hiyo kwa ukubwa.

Kompany aliwasuta watesi wake baada ya ushindi mnono wa mabao 9 kwa 2 dhidi ya Dinamo Zagreb katika mechi ya klabu bingwa barani Ulaya usiku wa Septemba 17.

Kocha huyo alisimulia jinsi alivyozaliwa jijini Brussels Ubelgiji kwa baba mzazi aliyekuwa mkimbizi kutoka Kongo. Simulizi hiyo kulingana na Kompany ilikuwa vigumu kuafikia mafanikio aliyojizoelea ila hatimaye alifanikisha.

"Je kuna nafasi gani kwangu hata kucheza kwenye ligi ya premia, kushinda kitu kama mchezaji, kuchezea timu ya taifa? Uwezekano ulikuwa 0.000. Sasa mimi ni kocha."  Alisema Kompany.

Vincent Kompany aliuliza, " Unawacha kujiamini na mambo unayoweza kufanikisha kwa sababu ya mambo wanayosema watu wengine?"

Aidha mshambulizi huyo wa zamani wa Mnachester City alisema kuwa mawazo  ameyaelekeza kuendeleza ushindi na ikiwa atafeli basi atafeli na akishinda atakuwa hakika ameshinda lakini anaweza boreka kila uchao.

Harry Kane alifunga mabao manne , Michael Olise akafunga mawili na Raphael Guerriro, Leroy Sane na Leon Goretzka wakafunga bao moja kila mmoja.

Dinamo Zagreb walipata mabao ya kufutia machozi kupitia wachezaji Bruno Petkovic na Tekuya Ogiwara.

View Comments