In Summary

• Uwanja mpya katika mkoa wa mitaa ya Arusha utatumika kwa mazoezi wakati wa AFCON ya 2027.

• Kenya, Tanzania na Uganda zilikubaliwa kuandaa michuano ya AFCON ya mwaka 2027 kwa pamoja.

Uwanja wa Benjamin Mkapa, Tanzania
Image: HISANI

Usimamizi wa mkoa wa Arusha unapania kujenga uga mwingine wa michezo kuanzia Oktoba katika matayarisho ya maandalizi ya kuandaa AFCON 2027 kwa ushirikiano na Kenya na Uganda.

Uwanja huo mpya utajengwa katika jiji la Arusha kwenye eneo la Burka karibu na sehemu ambapo taifa la Tanzania linajenga uwanja mwingine utakaotumika mwaka wa 2027 katika AFCON.

Takribani sehemu ya shamba lenye ukubwa wa ekari nane umetengwa na mamlaka ya mkoa wa Arusha kulingana na taarifa ya afisa wa michezo mkoani humo Bw, Priscus Silayo.

Ikiwa uwanja huo utakamilika kufikia  mwaka wa 2027, utatumika katika shughuli za mazoezi na matayarisho ya kabla ya mechi za AFCON.

Kenya, Tanzania na Uganda zilikubaliwa kuandaa michuano ya AFCON ya mwaka 2027 kwa pamoja.

Taifa la Kenya lipo mbioni kukarabati viwanja wa kujenga kiwanja kipya cha Talanta ambapo kinatarajiwa kuwa kitatumika katika ufunguzi wa kipute cha AFCON na kutumika kwa mechi ya fainali.

Viwanja vya Kasarani na Nyayo vinakarabatiwa.

Katika taifa la Tanzania, tayari kiwanja cha Benjamin Mkapa kliiidhinishwa kutumika. Nchini Uganda, kiwanja vya St. Marys na uwanja wa kitaifa wa Mandela  vitatumika.

View Comments