In Summary

• Uwanja wa Kirigiti ulianza kujengwa miaka minne iliyopita lakini unakaribia kukamilika baada ya Waziri Murkomen kukagua ujenzi huo.

• Waziri ameomba washikadau katika sekta ya kibinafsi kuwekeza katika vifaa vya michezo kote nchini.

Waziri wa michezo Kipchumba Murkomen alipozuru uwanja wa Kirigiti mnano Ijumaa, Agosti 20, 2024
Image: X// Waziri Kipchumba Murkomen

Waziri wa michezo Kipchumba Murkomen amesema kuwa ujenzi wa uwanja wa KIrigiti unakaribia kukamilika na hivi karibuni.

Uwanja huo sasa umebakisha kuwekwa viti, kuanzishwa kuwekewa miundombinu ya teknolojia pamoja na kumaliza kutengeneza sehemu ya kuchezea.

Uwanja wa Kirigiti unajulikana sana eneo la kati mwa Kenya kuwa sehemu ambayo rais mwanzilishi wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta alihutubu mara ya mwisho kabla ya kufungwa jela katika eneo la Lokitaung.

Waziri Murkomen ameridhishwa na hatua ambazo ujenzi wa uwanja huo umefikia akiwataka washikadau katika sekta za kibinafsi kuwekeza katika kiwanja hicho.

Ujenzi wa uwanja wa Kirigiti uling'oa nanga miaka minne iliyopita wakati wa utawala wa rais mstaafu Uhuru Kenyatta na kufikia sasa ungali unaendelea kujengwa.

Ni kinaya namna ujenzi huo haujakamilika miaka minne baadaye ilhali serikali ya rais William Ruto ilimhakikishia rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF Patrice Motsepe kuwa uwanja mpya wa Talanta City utakamilika kabla ya 2027. 

Ujenzi wa uga wa kimataifa wa Talanta City ulianza mwaka  wa 2024 na uatarajiwa kukamilika kufikia Desemba 2026 kwa ajili ya kuanda AFCON ya mwaka 2027. Kumaanisha unajengwa kwa miaka miwili tu.

Hata hivyo, kumalizika kwa ujenzi wa Kirigiti haujabainika.

Waziri Murkomen amesema kuwa atafanya mkutano na shirika la serikali la Sports Kenya kujadili tarehe ya kukamilika kwa ujenzi huo.

 

 

View Comments