In Summary

• Picha za wachezaji wa AFC Leopards zilisambaa mtandaoni wakivalia jezi zao katika sehemu wazi kwenye mechi ya ligi kuu nchini.

• Trucha amewataka washikadau husika kufuata sheria za mechio kuandaliwa katika uwanja ulio na mazingira bora.

Image: HISANI

Kocha wa klabu ya AFC Leopards Tomas Trucha amelalamikia hali mbovu ya uwanja wa Thika ambao unatumika katika soka.

Malalamishi ya kocha Trucha yanajiri baada ya mechi ya AFC Leopards ugani humo mnamo Jumamosi 21  dhidi ya Bidco United ambapo walishinda mchuano huo kwa bao moja.

Picha zilisambaa mtandaoni za wachezaji wa AFC Leopards wakivalia jezi zao katika sehemu wazi kwani uwanja huo hauna chumba maalum cha wachezaji kubadilishia mavazi yao.

Kocha Trucha amesema kuwa uwanja wa Thika kamwe haufai kutumika katika mechi za ligi kuu nchini kwa kuwa zinakosa vyumba vya kuvalia na vyoo.

Kocha huyo raia wa Jamhuri ya Czech amelalamika kuwa hakufurahia mechi uwanjani Thika akiwataka washikadau husika kufuata maagizo ya kupanga mechi kuchezea kwenye viwanja bora.

"Mnahitaji kufuata sheria, Unahitaji vyumba vya kuvalia. Ukitaka kujisaidia,unaenda wapi?" Aliuliza Trucha.

Kutokana na ukarabati unaoendelea katika uwanja wa Kasarani na ukarabati unaotarajiwa kuanza katika uga wa Nyayo, shirikisho la soka nchini FKF lilitoa orodha ya viwanja mbadala.

Viwanja hivo ikiwemo uwanja wa Thika vilistahili kutumika kuandaa michuano ya ligi kuu nchini Kenya.

View Comments