logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Man United yamsajili kipa wa Cameroon, Andre Onana baada ya mkataba wa De Gea kumalizika

Hapo awali aliwahi kufanya kazi na kocha wa Man United Erik ten Haag katika Klabu ya Ajax nchini Uholanzi.

image
na Radio Jambo

Habari21 July 2023 - 04:22

Muhtasari


•Mashetani Wekundu walithibitisha usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Inter Milan ya Italia siku ya Alhamisi.

•Hapo awali aliwahi kufanya kazi na kocha wa Man United Erik ten Haag katika Klabu ya Ajax nchini Uholanzi.

Klabu ya soka ya Uingereza, Manchester United imetangaza kumsajili mlinda mlango wa timu ya taifa ya Cameroon Andre Onana.

Mashetani Wekundu walithibitisha usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Inter Milan ya Italia siku ya Alhamisi kupitia kurasa rasmi za klabu hiyo.

"Andre Onana amejiunga na Manchester United kwa kandarasi inayoendelea hadi Juni 2028, na chaguo la mwaka zaidi, kibali cha kimataifa kinasubiriwa," taarifa ya Man United siku ya Alhamisi jioni ilisoma.

Klabu hiyo pia ilithibitisha kuwa Onana atavaa jezi namba 24 akiwakilisha Mashetani Wekundu katika msimu wa 2023/24 unaoanza mwezi ujao.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Cameroon hata hivyo bado hajaripoti katika maskani yake mapya, Old Trafford kwani kuna baadhi ya taratibu ambazo hazijakamilika.

Wakati akizungumza baada ya kuthibitishwa kwa usajili wake katika United, Onana alisema ni heshima kubwa kusajiliwa na klabu hiyo ya EPL na kuweka wazi kwamba anafurahia sana safari yake mpya.

"Kujiunga na Manchester United ni heshima kubwa na nimefanya kazi kwa bidii maisha yangu yote kufikia wakati huu, kushinda vikwazo vingi njiani. Kuenda Old Trafford ili kulinda lengo letu na kuchangia timu itakuwa uzoefu mwingine wa kushangaza. Huu ni mwanzo wa safari mpya kwangu, na wachezaji wenzangu wapya, na matamanio mapya ya kupigania,” alisema.

Aliongeza, "Manchester United ina historia ndefu ya makipa wa ajabu, na sasa nitatoa kila kitu kuunda urithi wangu mwenyewe katika miaka ijayo. Nimefurahishwa na nafasi ya kufanya kazi tena na Erik ten Hag, na siwezi kusubiri kucheza sehemu yangu katika mafanikio ninayojua amedhamiria kutimiza katika klabu hii kubwa ya soka.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ni mmoja wa makipa wenye viwango vya juu katika ulimwengu wa soka kwa sasa na amekosa kufungwa katika jumla ya mechi 104 katika mechi 255 alizocheza na klabu.

Hapo awali aliwahi kufanya kazi na kocha wa Man United Erik ten Haag katika Klabu ya Ajax nchini Uholanzi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved