In Summary

•Real Madrid imetangaza kuwa nahodha wake Karim Benzema ataondoka kufuatia mwisho wa msimu wa 2022/23.

•Kuna tetesi kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 anaondoka Uhispania ili kujiunga na ligi ya Saudi Arabia.

Image: TWITTER// KARIM BENZEMA

Klabu ya Real Madrid imetangaza kuwa nahodha wake Karim Benzema ataondoka kufuatia mwisho wa msimu wa 2022/23.

Katika taarifa ya Jumapili, klabu hiyo ya Uhispania ilitangaza kuwa hafla maalum ya kumuaga mshambuliaji huyo itafanyika Jumanne.

"Jumanne ijayo 6 Juni, saa sita adhuhuri (CEST), tukio la kitaasisi la kumuenzi na kumuaga Karim Benzema litafanyika kwenye Uwanja wa Real Madrid Sport City, ambalo litahudhuriwa na rais wetu, Florentino Pérez," taarifa hiyo ilisema.

Washindi hao wa Laliga msimu wa 2021/22 walitangaza kuwa Benzema amepata haki ya kuamua hatua yake ijayo.

"Real Madrid ingependa kuonyesha shukrani zetu na upendo kwa mchezaji ambaye tayari ni mmoja wa magwiji wetu wakubwa," ilisema taarifa hiyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alijiunga na Real Madrid mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 21.

Tangu ajiunge na klabu hiyo, ameshinda Vikombe 5 vya Uropa, Vikombe 5 vya Kombe la Dunia la Klabu, Vikombe 4 vya Super Cup, Ligi 4, Vikombe 3 vya King’s Cup na 4 vya Super Cup za Uhispania.

Kuna tetesi kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 anaondoka Uhispania ili kujiunga na ligi ya Saudi Arabia.

Wiki jana, mwenzake wa zamani katika Real Madrid, Christiano Ronaldo,  ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia alizungumzia tetesi za yeye kujiunga na ligi hiyo.

"Wanakaribishwa, ligi itaimarika, na kwa sasa ina wazuri wa kigeni na Waarabu," alisema.

Benzema hata hivyo bado hajafichua mipango yake ijayo.

View Comments