logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tazama orodha mpya ya FIFA ya timu 20 bora Duniani baada ya Kombe la Dunia

Argentina imepanda kutoka nafasi ya tatu hadi nafasi ya pili

image
na Samuel Maina

Michezo20 December 2022 - 05:43

Muhtasari


  • •Brazil wamesalia kileleni licha ya kubanduliwa nje ya Kombe la Dunia katika hatua ya robo fainali.
  • •Ufaransa wamepanda kutoka nafasi ya nne hadi ya tatu huku Ubelgiji wakishuka ngazi mbili hadi nafasi ya nne.

Argentina imepanda kutoka nafasi ya tatu hadi nafasi ya pili kwenye orodha ya timu bora za soka duniani baada ya kushinda Kombe la Dunia nchini Qatar siku ya Jumapili, sasa imefichuliwa.

Kulingana na orodha mpya ya FIFA iliyoratibiwa kutolewa rasmi siku ya Alhamisi, mahasidi wao wakubwa Brazil wamesalia kileleni licha ya kubanduliwa nje ya Kombe la Dunia katika hatua ya robo fainali.

Washindi wa pili wa Kombe la Dunia 2022, Ufaransa wamepanda kutoka nafasi ya nne hadi ya tatu huku Ubelgiji wakishuka ngazi mbili hadi nafasi ya nne. Uingereza imesalia katika nafasi ya tano.

Hii hapa orodha ya timu bora 20 mwaka wa 2022:-

1) Brazil

2) Argentina (+1)

3) Ufaransa (+1)

4) Ubelgiji (-2)

5) Uingereza

6) Uholanzi (+2)

7) Croatia (+ 5)

8) Italia (-2)

9) Ureno

10) Uhispania (-3)

11) Moroko (+11)

12) Uswizi (+3)

13) Marekani (+3)

14) Ujerumani (-3)

15) Mexico (- 2)

16. Uruguay (-2)

17. Colombia

18. Denmark (-8)

19. Senegal  (-1)

20. Japan (+4)


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved