In Summary

•Mashindano ya raga ya wachezaji 7 kwa wanaume yatachezwa kati ya Julai 24-27, wakati mashindano ya wanawake yakifanyika Julai 28-30.

•Mabingwa watetezi New Zealand, wako katika Pool A pamoja na Ireland, Afrika Kusini, na Japan.

Image: TWITTER// SHUJAA 7S

Timu ya raga ya wachezaji saba,Shujaa wamejumuishwa kwenye kundi B  mashindano ya Olimpiki kule Paris 2024 pamoja na mabingwa wa world seven Series Argentina,Australia na Samoa.

Kenya ambayo inashiriki kwa mara ya tatu mfululizo kwenye mashindano ya kimataifa katika toleo fupi la mchezo huo inakabiliwa na mtihani mzito katika shindano hilo la siku tatu.

Kocha wa Shujaa,Kevin Wambua atatafuta nafasi ya kupanda jukwaani baada ya mashindano mawili ambayo hayakufaulu wakati wa hafla ya Rio mnamo 2016 na Tokyo 2020 .

Mabingwa watetezi New Zealand, wako katika Kundi A pamoja na Ireland, Afrika Kusini, na Japan. Pool C inashirikisha mabingwa wa 2016 na 2020 Fiji, wenyeji Ufaransa, Marekani na Uruguay.

Mashindano hayo  kwa wanaume yatachezwa kati ya Julai 24-27, wakati mashindano ya wanawake yatafanyika Julai 28-30. Kwa mara ya kwanza, mechi za raga ya wachezaji saba zitaanza siku mbili kabla ya sherehe ya ufunguzi, kwa wanaume hatua ya awali na robo fainali.

Mwenyekiti wa Raga Ulimwenguni, Sir Bill Beaumont alisema: “Tunafuraha kuzindua makundi ya Olimpiki ya wachezaji saba saba kwa kile kinachoahidi kuwa mashindano ya kizamani kwa mchezo wetu katika mji mkuu wa Ufaransa.

View Comments